DAWASA yaruka kiunzi cha Magufuli

0
Waziri wa Maji, Juma Aweso, akizindua bomba la maji, Kifuru jijini Dar es Salaam, hiyo ikiwa ni ishara ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais John Magufuli ya kutaka kukamilishwa miradi yote ya huduma ya maji.

NA SHEHE SEMTAWA

KUTOKANA na agizo la Rais Dk. John Magufuli la kuitaka Mamlaka ya Maji safi na Majitaka Dar es salaam (DAWASA) kufikisha huduma ya Maji safi kwa wakazi wa Jimbo la Ukonga na Segerea kabla ya Disemba 25 Mwaka huu, hatimaye mradi ya tenki la kusambaza maji katika maeneo hayo limekamilika.

Mapema jana Waziri wa Maji Jumaa Aweso alishuhudia ukamilishaji wa Mradi wa Ujenzi wa Tanki kubwa la Maji linalopokea maji kutoka Kisarawe kwenda Pugu lenye uwezo wa kupokea na kusambaza Lita milioni 2.8 kwa siku.

Mradi huo una thamani ya Sh. bilioni 6.9 ambapo tankI hilo jana lilianza kupokea maji na kuyasambaza kwa wananchi.

Maji hayo yalianza kutumika kwa wananchi wa baadhi ya maeneo ya Kinyerezi ambao walikuwa wakisubiri kukamilika kwa mradi huo wa maji wa Kisarawe-Pugu-Gongolamboto.

Mradi huo utahudumia pia wakazi wa Jimboa Ukonga ikiwemo Pugu, Majohe, Gongolamboto, Bangulo, Airwing, Kigogo, Chanika, Kinyamwezi, Banana na Kifuru.

Aidha, Aweso, alimpongeza, Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Luhemeja kwamba anafanya kazi nzuri na kumtaka kuendelea kufanya kazi “bila kujali vita unayopigwa na baadhi ya watu.”

“Unafanyakazi kubwa sana kafanye nilizungumza ofisini na hapa nazungumza usiogope, fanya kazi, mtangulize Mungu mbele.

“Hiki kitu ulichowafanyia wananchi na hili agizo la Rais Magufuli, leo wananchi hawa wanapata maji hii ni Baraka kubwa zaidi, kikubwa tunataka wakurugenzi, wahandisi wote wa maji twendeni tukatatue tatizo la maji.

“Watanzania wanataka maji si blabla na maneno na sisi kama viongozi tutalisimamia hilo, katika kuhakikisha kwamba Watanzania wanapata huduma ya maji,”alisema Aweso.

Mabli na kupongeza jitihada zinazofanyika  Waziri Aweso aliitaka DAWASA kufanya mabadiliko makubwa katika sekta hiyo.

“Si Mamlaka ya tu ya Dar es Salaam, mamlaka zote na maeneo yote ya Tanzania yanayohusiana katika suala zima la maji kuna maeneo mengine wakati mwingine watu wanajisahau ofisini mtu akishapigwa na kiyoyozi kwamba kuna shida.

“Shida hazitatuliwi kwenye laptop anaye lala na mgonjwa ndiye anayejua mihemo ya mgonjwa, nenda huko ukaone shida ili uweze kwenda kuzitatua.

“Kwa hiyo tunakutaka kama Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam, fanya mabadiliko kwa mameneja wote katika mikoa hii ya Dar es Salaam ili kuhakikisha kwamba tunakwenda kuboresha huduma ya maji katika jiji la Dar es Salaam,”alisema Aweso.

Katika hatua nyingine Aweso, aliwatumia salamu Watalamu wa waizara yake na wa mamlaka zote za maji nchini kuwa wasijifanye kuwa wamezizoea shida za wananchi.

Aweso, alisema lazima wataalam hao wajitume katika kuhakikisha kuwa wanasimamia miradi hiyo kwa matengezo mara wanapopata taarifa kutoka kwa wananchi amabao ndio waajiri wa watendaji wa mamlaka hiyo.

“Lingine ambalo nadhani nitume salam, Wataalam wa Wizara ya Maji, Wataala wa Mamlaka zote za maji nchini, tusizoe shida za wananchi.

“Si vema hata kidogo au ijengeke tabia kuona mwananchi wa kijijini kunywa maji na punda, kunywa maji na mifugo ikawa ni haki yake la hasha.

“Isijengeke tabia kuona pesa ambazo zinapelekwa na wizara ambazo tumepewa na mheshimiwa Rais John Magufuli watu kujitafunia tafunia au kijanja janja, wanakula pesa za miradi ya maji la hasha,”alisema Aweso.

Aweso, aliwataka wataalamu hao, kuzifanyia kazi taarifa za hitilafu kama vile kuvuja bomba, mara wazipatapo kutoka kwa wananchi.

“Isijengeke tabia kumuona mwananchi wa kawaida, leo wananchi wa Pugu, leo mradi umejengeka yawezekana kuna hitilafu ndogo bomba linavuja anatuma ujumbe mje kukarabati hakuna mtu ambaye hata kumjibu.

“Hakuna majibu yeyote ambayo katika kuhakikisha inatatua tatizo la maji, isijengeke tabia leo mwanchi huyu ambaye anajiunga bando na anarekodi anatuma kwamba hapa kuna mvujo ili aweze kupata huduma ya maji, lakini hakuna majibu yeyote.

“Niwambie wazi tu kuwa hatuwezi kuvumilia mambo ya namna hiyo nan i mambo ya ajabu sana meseji hiyo hiyo, ambayo anakutumia wewe mtaalam ambaye unalipwa mshahara kutokana na makusanyo ya huyo huyo mteja wako.

“Lakini Meseji haijibiwi, leo anatuma kwa Naibu waziri, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, akitumiwa katika group lile lile ambalo mwananchi yule yule, mnatoka na mavifaa na kwenda kulifanya jambo kwa haraka, mna tumia clip kwa waziri.

“Tunataka jitihada ambazo zinazo fanywa na viongozi, tunataka mkafanye vile ambavyo sisi tunataka na nyinyi kama mwananchi anavyotaka.

“Mwananchi ni bosi wako, na bosi siku zote hanuniwi tunataka mkafanye kazi kubwa kwa wananchi wetu, tunataka tukafanye kazi kubwa katika jiji letu,”alisema Aweso.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kunenge, alimshukuru Waziri kwa kuweka muongozo wa kusambaza maji yaweze kufikia wananchi kwa wakati.

“Mimi niseme naungana na wewe kabisa kwa utendaji mzuri wa DAWASA, bado tuna change moto baadhi ya maeneo lakini kweli DAWASA wanajitahidi hasa wanapotumia mapato yao ya ndani kujenga miradi.

“Sasa mimi niwaombe wakazi wa Dar es Salaam, wakazi wa kaka yangu Ndikilo ambapo pote pale DAWASA inatoa huduma naambiwa mpaka Morogoro sasa kwa ndugu yangu, kaka yangu Lowata.

“Tuhakikishe wananchi tunalipa bili za maji kwa wakati nafahamu DAWASA mmefanyakazi kubwa ya kuhakikisha bili zinakuwa sawa sawa na sahihi, endeleeni kuhakikisha bili ni sahihi.

Aliwataka wananchi walipe bili zao za huduma hiyo ya maji ili kuwawezesha DAWASA kufanya mambo makubwa zaidi katika kusambaza huduma hiyo muhimu ya maji.

Akizungumzia mradi huo pindi utakapokamilika Februa mwakani, Mhandisi Luhemeja, alisema gharama za mradi huo ni  Sh. Bil. 7 bila VAT fedha zote za mradi huo ni za ndani za DAWASA.

Pia alisema, maeneo yatakayonufaika na mradi huo ni Pugu, Majohe, Gongolamboto, Ukonga, Kigogo, Chanika, Buyuni, Pugu-Machimbo, Pugu Station na Mnadani.

Maeneo mengine ni Bangulo, Mongolandege, Kinyerezi na Ukonga Airwin.

 Aidha, Mhandisi Luhemeja, alisema mradi huo, ni miongoni mwa miradi ya kimkakati iliyopangwa na sasa unatekelezwa na DAWASA 2020/2021 ili kuweza kutekeleza maelekezo ya Serikali la kuhakikisha ifikapo 2020/21 upatikanaji wa maji wa huduma ya maji unafikia asilimia 85 na 95 kwa maeneo ya vijini na mijini sawia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here