DAWASA mshindi wa pili katika kipengele cha Mamlaka za maji Tuzo za NBAA

0

Na Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) imekuwa mshindi wa pili Tuzo ya umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2019 (Best Presented Financial Statements for the Year 2019 Awards) katika kipengele cha Mamlaka za maji.

Hafla ya utoaji wa tuzo hizo zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) zilifanyika jana Jumamosi Disemba 05, 2020 katika Kituo cha Mikutano cha NBAA Bunju jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi wa Fedha wa DAWASA. CPA Sais Kyejo alisema imekuwa ni mara ya kwanza wao kushiriki katika tuzo hizo na wamefanikiwa kushika nafasi ya pili.

Mkurugenzi wa Fedha wa DAWASA, CPA Sais Kyejo akizungumza na wanahabari

Kyejo alisema, kushika kwa nafasi hiyo kunaonesha wahasibu wanajua  kazi wanayofanya na wanazingatia viwango; “Kupata kwa tuzo hii kuna maana kubwa sana kwa taasisi yetu sambamba na wahasibu waliopo kwenye idara ya fedha.”

Alisema wanahidi kuendelea  kuwa katika Viwango bora kila siku kwani kupata kwa tuzo hiyo kumeleta chachu kwenye taasisi na idara nzima.

“Leo tuna furaha sana kwasababu tumepokea tuzo ya hesabu zilizoandaliwa vizuri kwa mwaka 2019, hii ni mara yetu ya kwanza kupokea tuzo hii kama Taasis tuna furaha kuona kwamba wahasibu ambao tunao wanajua kuandaa hesabu vizuri na inaonesha Taasis inazngatia viwango vya ubora wa uaandaaji wa hesabu.

“Tuzo hii ina maana kubwa sana kwa Taaisis na kwetu sisi Wahasibu kwamba sasa tunaweza kuendana na viwango vya Kimataifa vya uandaaji wa hesabu, itatusaidia kuhakikisha kwamba tunaendelea kudumisha viwango vya huduma zetu.

“Tumeshiriki kwa mara ya kwanza na tumeweza kufanya vizuri na hili linaleta chachu katika taasisi yetu na idara nzima na tutahakikisha mwaka huu tunaandaa hesabu zetu vizuri ili mwaka ujao tufanye vizuri zaidi na hata tuwe washindi wa kwanza,” alisema CPA Kyejo.

Tuzo ya DAWASA ilipokelewa Na Afisa Mtendaji Mkuu wa mamlaka hiyo, Mhandisi Cyprian Luhemeja akiambatana na watumishi wengine wa Mamlaka.

Baadhi ya watumishi wa DAWASA wakiwa picha ya pamoja baada ya kushinda Tuzo.

Mshindi wa kwanza katika kipengele cha Mamlaka za Maji alikuwa Mamlaka ya Majisafi na Salam Tanga (UWASA) na mshindi wa tatu akiwa ni Mamlaka ya Maji  Iringa (IRUWASA).

Aidha mshindi wa jumla katika Tuzo alikuwa ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ikiwa ni Mara ya tatu mfululizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here