Dawasa, Ewura zakutana kutatua changamoto za huduma Kigamboni

0
Meneja Mawasiliano wa DAWASA, Everlasting Lyaro, akizungumza katika mkutano huo

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar-es-salaam (DAWASA) pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imekutana na wananchi wa wilaya ya Kigamboni kutoa elimu na kupokea changamoto za kihuduma.

Mkutano huo uliohudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri ambaye ametoa wito kwa taasisi za Serikali kujenga tabia ya kuongea na kuwasiliana na wananchi kila wakati ili kuongeza ufanisi na kupunguza malalamiko.

Awali akimkaribisha Mkuu wa Wilaya, Meneja wa DAWASA Kigamboni Tumaini Mhondwa amesema vyanzo vikuu vya maji katika wilaya ya Kigamboni ni visima na maji kutoka mtambo wa Ruvu Chini zinahudumia kata sita ambazo ni Somangira, Kisarawe II, Vijibweni, Mji mwema, Kigamboni pamoja na Tungi.

Meneja wa DAWASA Kigamboni, Tumaini Mhondwa.

Ameongeza kuwa kata zilizobaki ambazo ni Pemba Mnazi, Kimbiji na Kibada zinategemea kunufaika na huduma ya Majisafi baada ya kukamilika kwa mradi wa visima vya Kimbiji.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa EWURA kanda ya Mashariki Mhandisi Amani Nyekere amewasisitizia wananchi kutumia wataalamu pindi wanapoomba huduma katika makazi yao ili kuepuka hasara ya kupasuka kwa mabomba itakayopelekea gharama kubwa ya ankara za maji.

Katibu Tawala Manispaa ya Kigamboni, Dalmia Mikaya akizungumza katika mkutano huo.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here