Dakika 60 za mazungumzo mazito Magufuli, Xi Jinping

0

NA GERSON MSINGWA, IKULU

Rais wa China , Xi Jinping amempigia simu rais Dk John Magufuli na kufanya mazunguzmo kuhusu kuimarisha zaidi uhusiano na ushirtikiano kati ya Tanzania hususani katika masuala ya uchumi.

Katika mazunguzmo hayo yaliyodumu kwa muda was aa moja Rais Jinping alimpongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa kipindi kingine cha pili na kueleza kuwa kuchaguliwa kwake kumetokana na kazi nzuri aliyoifanya katika kipindi cha miaka mitano ya kwanza ambapo uchumi umeimarika zaidi na kwamba anaiona Tanzania kuwa nchi itakayoongoza kwa ukuaji uchumi barani Afrika.

Aidha Rais Jinping alimpongeza Rais Magufuli kwa namna Tanzania ilivyokabiliana na ugonjwa wa Korona na kueleza jinsi China inavyoendelea kukabilianana ugonjwa huo.

Pia al;impongeza Rais Magufuli kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (SGR) na ujenzi wa bwawa la kuzalisha Megawati 2115 za umeme katika mto Rufiji.

Alieleza kuwa China itaangalianamna ya kushirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa miradi hiyo mikubwa.

Kwa upande wake Rais Magufuli alimshukuru Rais Jinping kwa kumpigia simu, kumpongeza kwa kuchaguliwa kwake kwa kipindi cha pili na kumpongeza kwa hatua za kimaendeleo zinazopigwa na Tanzania hasa katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati.

Rais Magufuli alimhakikishia Rais Jinping kuwa Tanzania itaendelea kukuza zaidi ushirikiano wake na China uliodumu kwa takribani miaka 55 baada ya kuahasisiwa na Baba wa Taifa Hayati, Mwl. Julius Nyerere na Hayati Mwenyekiti Mao Zedong  na kwamba Tanzania itanedlea kuiunga mkono China katika mambo mbalimbali ya kimataifa.

Rais Magufuli alisema katika mazungumzo hayo kuwa Tanzania inawakaribisha wafanyabiasha na wawekezaji kutoka China kuja kuwekeza katika maeneo mabalimbali ya uzalishaji , utalii, ujenzi kwa manufaa ya pande zote mbili.

Adha Rais Magufulia aliiomba China kushirikana na Tanzania katika utekelezaji wa miradi mikubwa kwa kutoa mikopo nafuu.

Aliitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni kuzalisha megawati 358 za umeme katika mto Ruhudji, Megawati 222 za umeme katika mto Rumakali na ujenzi wa Barabara visiwani Zanzibar.

Kadhalika Rais MAgufuli aliiomba China kufungua zaidi masoko ya bidhaa mbalimbali ktoka Tanzania hususani mazao ya kilimo.

Rais Jinping aliahidi kufanyia kazi maombi yaliyotolewa na Rais Magufuli ikiwemo ujenzi wa miradi ya kuzalisha umeme Ruhudji na Rumakali, ujenzi wa reli, Bwawa la Nyerere na ununuzi wa mazao ya Tanzania.

Rais wa Dk. John Magufuli akizungumza kwa njia ya Simu na Rais wa China
Xi Jinping Ofisini kwake Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma jana Disemba 15, 2020. PICHA NA IKULU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here