CUF yafufua mchakato wa Katiba mpya

0

Chama cha CUF jana kimezindua Kongamano la kudai Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi, ikiwa ni siku 53 baada ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania kufanyika.

Akifungua Kongamano hilo, Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba ametoa rai kwa Rais John Magufuli kuheshimu maoni ya wananchi kwa kuwapatia Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi.

Vilevile, amesema Rais anatakiwa kuheshimu ukomo wa Uongozi uliopo kwa mujibu wa Katiba na kuepuka majaribio yoyote ya kumuwezesha kukaa madarakani kwa muda mrefu.

Amesema Rais anapaswa kufufua mchakato ya kuandika Katiba mpya kuwapatia Watanzania Tume huru ya Uchaguzi itakayounganisha Taifa na kufuta machungu yaliyotokana na Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Ameongezaa kuwa, rasimu ya Katiba mpya iliyo chini ya Jaji Mstaafu Joseph Warioba imekidhi matakwa ya wananchi walio wengi na jukumu alilobaki nalo Rais ni kuhitimisha mchakato huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here