CUF kutoshiriki uchaguzi wowote kuanzia sasa

0

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 

CUF KUTOSHIRIKI UCHAGUZI WOWOTE KUANZIA SASA

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba amesema kuanzia sasa chama hicho hakitashiriki uchaguzi wowote na badala yake kitajikita katika harakati za kudai katiba mpya, ili kupatikana kwa Tume huru ya Uchaguzi itakayosimamia mchakato huo.

Profesa Lipumba ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari katika makao Makuu ya CUF Buguruni jijini Dar es Salaam.

“CUF inawaomba Watanzania wote wapenda haki nchini kufanya ibada Maalum siku ya Alhamis, ambapo tutafunga kwa kutokula mchana na tufanye dua na maombi kila mmoja kwa imani yake ili kumuomba Mungu apitishe hukumu ya haki kutokana na kile kilichotendeka katika uchaguzi ” Prof. Lipumba.

Prof. Lipumba alikuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020 ambapo akipata kura 72, 885.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here