#COVID_19: Ujerumani yazidiwa ICU

0

Ujerumani iko katika hatari ya kukumbwa na uhaba wa vitanda katika idara ya wagonjwa mahututi, ICU, iwapo visa vya virusi vya corona vitaendelea kuongezeka. Uwe Janssens, Daktari katika idara ya ICU na mjumbe wa Chama cha Huduma za wagonjwa Mahututi na Dawa za Dharura nchini Ujerumani, DIVI ameonya kuwa hali ni mbaya kwenye baadhi ya hospitali za nchi hiyo.

Janssens amesema kuna maeneo ambako idara ya ICU imebakiza vitanda vitano vilivyo wazi hadi asilimia 10. Amebainisha kuwa idadi hiyo haitoshi kuwahudumia wagonjwa walioko katika hali mbaya. Hata hivyo, amesema kwa sasa hospitali bado zina uwezo wa kuwahudumia wagonjwa, lakini maambukizi yakiendelea kuongezeka hilo halitasaidia.

Janssens amesema wataalamu wa afya kwenye idara za ICU nchini Ujerumani wanafanya kazi katika shinikizo kubwa. Visa vipya 28,438 vimeripotiwa nchini Ujerumani ndani ya saa 24.

✍#DW

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here