CCM yashinda ubunge Kibakwe kwa Simbachawene na Mpwapwa

0

Na Mwandishi Wetu

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amemetea kiti cha ubunge wa Jimbo la Kibakwe kwa kushinda kwa kura 37,626.

Msimamizi wa uchaguzi, Sweya Mamba amemtangaza Simbachawene kushinda ubunge leo 29, 2020 saa mbili usiku dhidi ya mpinzani wake wa Chadema, Msafiri Mzinga aliyepata kura 3,072.

Mamba amesema waliojiandikisha kupiga kura jimboni hapo ni 86,791, waliopiga kura ni 41,621 na kura zilizokataliwa ni 923.

Pia, Mamba amemtangaza mgombea ubunge wa CCM katika jimbo la Mpwapwa, George Nathan kuwa ameshinda ubunge kwa kupata kura 29,623.

Mamba amesema mgombea ubunge wa Chadema, Ezekiel Chisinjila amepata kura 5,989.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here