China yamuajiri Jaji Mkuu mstaafu wa Uganda

0

Mahakama ya Juu zaidi nchini China imemteua mwanasheria mkuu wa zamani wa Uganda,  kama mwanachama wa jopokazi la wataalamu wa kuamua mzizo ya biashara ya kimataifa.

Jaji Katureebe atahudumu katika kamati hiyo kwa kipindi cha miaka mine ijayo.

Alistaafu kutoka mahakama ya juu zaidi ya Uganda mwezi Juni baada ya kutimiza miaka 70 kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo.

“Nimefurahia sana uteuzi hu, kwasababu ni kamati ya ngazi ya juu ambayo itaimarisha taaluma yangu,” alinukuliwa na akisema katika taarifa iliyowekwa katika mtandao wa twitter wa idara ya mahakama ya Uganda.

Chama cha mawakili nchini Uganda pia kimempongeza Jaji Katureebe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here