Home AFYA CHINA: TAHARUKI YAIBUKA BAADA YA MTU MMOJA KUFARIKI KUTOKANA NA KIRUSI KIPYA...

CHINA: TAHARUKI YAIBUKA BAADA YA MTU MMOJA KUFARIKI KUTOKANA NA KIRUSI KIPYA CHA HANTA

NA MWANDISHI WETU

Kwa mujibu Gazeti la Mtandaoni la China, Global Times limeripoti kuwa mwanaume mmoja kutoka Mji wa Yunnan nchini humo amefariki kwa Virusi vya Hanta akiwa anarejea Shandong akiwa kwenye basi. Watu 32 waliokuwa ndani ya basi hilo wamefanyiwa vipimo vya virusi hivyo.‬

Kulingana na Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa na (CDC), Virusi vya Hanta ni familia ya virusi ambavyo huambukizwa na panya na inaweza kusababisha magonjwa mbalimbali kwa binadamu.

Inaweza kusababisha hata ugonjwa wa figo na ugonjwa huo hauambukizwi kwa njia ya hewa na huweza kuenea kwa binadamu ikiwa atapatwa na mkojo, kinyesi au mate ya panya na mara chache na kuaambukizwa kutoka kwa mtu aliyeambukizwa.

Ugonjwa wa Virusi vya Hanta unaripotiwa kipindi ambacho mataifa mengi duniani yameathiriwa na Virusi vya Corona ambayo vilianziwa Wuhan, China mwishoni mwaka jana na hadi sasa vimeua watu 17, 148 na kuathiri wengine 103, 235 duniani kote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -

Most Popular

Yanga yampatia Tshishimbi mkataba mpya

NA MWANDISHI WETU Klabu ya Yanga SC, imesema kuwa tayari imemaliza kazi yake ya kuhakikisha inambakiza kiungo tegemeo wa...

Tetesi za soka barani Ulaya

SANCHO AITIKISA UNITED Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Timu ya Taifa ya Uingereza, Jadon Sancho (20), amesema hatakuwa tayari...

Makonda: Wazururaji hawatakwenda mahabusu watazibua mitaro ya maji machafu

NA MWANDISHI WETU Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kuwa watu watakaokamatwa kwenye mkoa huo kutokana...

Chui katika hifadhi ya wanyama ya Bronx akutwa na Virusi vya Corona

NEW YORK, MAREKANI Chui wa kike wa Malaysia aliyefahamika kwa jina la Nadia mwenye umri wa miaka minne katika hifadhi...

Recent Comments