Cheyo awataka viongozi wa vyama vya siasa kuwa wazalendo

0

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Chama cha United Democratic (UDP), John Cheyo amewataka viongozi wa vyama vingine vya siasa kuepuka kutoa lugha zenye kuhamasisha kuwagawa wananchi bali watangulize kwanza uzalendo kwa Taifa la Tanzania na kutoa ushirikiano kwa Rais aliyechaguliwa kwa wingi na watanzania kwa maendeleo ya nchi.

Akizungumza na wanahabari Jijini Dar es salaam, Cheyo amesema sasa uchaguzi umekwisha iliobaki ni kuendelea kuchapa kazi na kujiandaa vyema na chaguzi nyingine zinazofuata kwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kujiandikisha katika daftari la kupiga kura ili waweze kuwa na sifa za kupiga kura muda utakapowadia.

Pamoja na mambo mengine Cheyo ameipongeza hotuba iliyotolewa na Rais Dk. John Magufuli aliyoitoa Novemba 5, 2020 alipoapishwa rasmi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba atashirikiana na vyama vingine katika kulijenga Taifa akibainisha kuwa licha ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushinda kwa kishindo bado Tanzania ni nchi inayoendeshwa kwa mfumo wa vyama vingi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here