Chanzo cha kifo cha MC Zipompapompa chatajwa

0

>>Wasema tuliita waumini wa Mungu kumuongoza sala ya toba

NA MWANDISHI WETU

MUIGIZAJI maarufu wa Bongo Movies, MC Zipompapompa amefariki dunia juzi Jumanne, Novemba 10, 2020 nyumbani kwake baada ya kuugua kwa siku chache.

Wakizungumza jijini Dar es Salaam jana, ndugu na marafiki wa karibu wa MC Zipompapompa wameeleza masikitiko yao kutokana na msiba huo ambao umekuwa wa ghafla sana kufuatia  kuugua kwa siku chache.

“Alikuwa anapumua kwa tabu, tukaenda kupima homa, malaria, UTI vyote alikuwa hana, tukapima presha tukakuta ana 160. Waumishi wa Mungu walikuja wakampa maombi na kumuongoza sala ya toba.

“Usiku majira ya saa nane akazidiwa akawa anapata tabu kupumua, nikamchukua ili kumpeleka hospitali; bahati mbaya akawa amefariki hapo nje kabla hatujaondoka kwenda hospitali,”alisema Lona, ambaye ni mtoto wa dada yake Zipompa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here