Chamuriho aagiza kituo cja ukaguzi wa pamoja Vigwaza kukamilika 2021

0
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mkoa wa Pwani, Mhandisi Wilicis Mwageni, alipokuwa akikagua maendeleo ya mradi wa Kituo cha pamoja cha Ukaguzi (OSBP), Mkoani Pwani .

NA DOTTO KWILASA,PWANI

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Dk. Leonard Chamuriho, amemwagiza Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Pwani kukamilisha mradi wa ujenzi wa kituo cha ukaguzi wa pamoja wa magari (One Stop Inspection Station) ifikapo mwezi machi 2021.

Akizungumza mara baada ya kukagua utekelezaji wa mradi huo, eneo la Vigwaza mkoa wa Pwani, Dakta. Chamuriho amesema kuwa kituo hicho ni njia mojawapo ya kurahisisha usafiri na ukaguzi wa mizigo inayoenda nje ya nchi pamoja na kutoa ajira kwa wananchi .

“Kupitia mradi huu wa ujenzi wa kituo cha ukaguzi wa pamoja wa magari hapa vigwaza utaleta ajira nyingi kwa wakazi wa hapa kama vile baba lishe, mama lishe na wafanyabiashara wengine watakaokuwa wanatoa huduma za ukaguzi na wasafirishaji”, amesisitiza Waziri Chamuriho.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi huo Mhandisi Mshauri Issack Shayo, alimueleza Waziri huyo kuwa tayari kazi za ujenzi imefikia asilimia 90 na hadi kufikia mwezi Februari mwaka hu ujenzi huo utakuwa umekamilika.

Naye Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Pwani Mhandisi Wilicis Mwageni, amesema kuwa utekelezaji wa mradi wa huo mpaka sasa miezi 15 imeshatumika na zaidi ya shilingi bilioni 9 zimetumika.

Katika hatua nyingine, Waziri Chamuriho amekagua kituo cha upimaji wa magari (MIZANI) cha mikese na upanuzi wa sehemu ya barabara ya Morogoro-Kingolwira yenye urefu wa meta 700 na kuwataka TANROADS Mkoa wa Morogoro kukamilisha kipande hicho hadi kufikia Februari mwaka 2021.

Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya sehemu ya mzani katika mradi wa Kituo
cha pamoja cha Ukaguzi (OSBP), Vigwaza Mkoani Pwani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here