Chadema waendeleze maigizo, sisi tunafanya kazi- Dk. Abbas

0

Na Mwandishi Wetu

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbas amesema Watanzania wamemaliza Uchaguzi na sasa wanaendelea na michakato ya demokrasia, kisheria na kikatiba ya kujenga Taasisi za nchi Ili kazi iendelee na kamwe hawawezi kupoteza muda na ‘maigizo’ ya baadhi ya viongozi wa upinzani hasa wa Chadema (Chama cha Demokrasia na Maendeleo).

Dk. Abbas Ameyasema hayo leo Novemba 10, 2020 wakati wa mahojiano yake na Shirika la Utagazaji la Uingereza (BBC).

“Hivi ninavyoongea mchakato unaofuata ni Bunge kuanza, watachagua Spika, watapelekewa Jina la Waziri Mkuu kumthibitisha na kisha Rais atazindua Bunge,” hao walioshindwa uchaguzi na kuanza tuhuma ni maigizo yao ambayo tumeyazoea kila mara wanaposhindwa” amesema.

Akijibu madai ya baadhi ya viongozi wa Chadema akiwamo Tundu Lissu na Godbless Lema wanaodai kuhofia Usalama wao na hata kujaribu kuomba Hifadhi ya ukimbizi nje ya nchi, Dk. Abbas amesema anashangazwa na hizo habari na kuhoji; wametishiwa usalama na nani, wapi na lini?

”Mkataba wa Kimataifa wa mwaka 1951 unaohusu Haki Na Hadhi za Wakimbizi kwa mfano unainisha bayana taratibu za kuwa mkimbizi, huwezi kuamka asubuhi tu ukajitangazia wewe ni mkimbizi au una kesi ya jinai ukataka kukimbia nchi kisa kudai ukimbizi.

“Mtu anaibuka anadai ametishiwa maisha lakini juzi katoka kushiriki kampeni siku 60 na amelindwa salama kabisa, leo kashindwa anakwambia anahofia maisha. Mkimbizi gani anavuka mpaka mbele kaandaliwa gari ya kumchukua? Haya ni maigizo.” amesema.

Aidha amesisitiza kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kuenzi misingi ya amani na kuwataka Watanzania kuendelea kuchapa kazi; “anayehofu Usalama wake atoe taarifa kwenye vyombo vya dola, wananchi waache na maneno ya watu waliokosa kuaminiwa na umma sasa wanatafuta kuonewa huruma.”

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here