CCM yaendelea kung’ara matokeo ya ubunge

0

Na Waandishi Wetu

Matokeo ya ubunge yanayoendelea kutangazwa leo Alhamisi Oktoba 28, 2020 yanaonyesha wagombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuibuka na ushindi katika majimbo mengi.

 Jimbo la Nkenge

 Katika jimbo la Nkenge wilayani Misenyi Mkoa wa Kagera msimamizi wa uchaguzi Innocent Mukandara amemtangaza mgombea wa CCM, Frolent Kyombo kuwa mshindi baada ya kupata kura 58,051 akifuatiwa na Magreth Kyai wa Chadema aliyepata kura 4,803. Katika jimbo hilo mgombea wa ACT-Wazalendo Leonard Kabakama amepata  kura 621 huku Leonard Leopord wa CUF akipata kura 179.

 Wanging’ombe

 Katika jimbo la Wanging’ombe Dk Festo Dugange wa CCM amepata kura  38,988, Adrea Luhwago wa Chadema amepata kura 4,381. Katika jimbo hilo kata 11 wagombea wa CCM walipita bila kupingwa huku moja ikichukuliwa na Chadema.

Muhambwe

 Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Muhambwe, Diocles Lutema amemtangaza Atashasta Nditiye wa CCM kuwa mshindi kwa kupata kura 29, 837. Felix Mkosamali wa Chadema ameshika nafasi ya pili kwa kupata kura 15,248 na Julius Masabo wa ACT Wazalendo kura 2,996.

 Rombo

 Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Rombo, Godwin Chacha, amemtangaza Profesa Adolf Mkenda (CCM) kuwa mshindi  baada ya kupata kura 48,122 kati ya kura  61,111 zilizopigwa.

 Mgombea wa Chadema, Patrick Asenga amepata kura 9,519 akifuatiwa na Jafet Masawe ACT-Wazalendo aliyepata kura  1,564  na Joseph Selasini wa NCCR-Mageuzi akipata kura 416.

Tarime mjini

 Ester Matiko wa Chadema ameshindwa kutetea ubunge baada ya kushindwa na mgombea wa CCM, Michael Kembaki.

 Msimamizi wa uchaguzi katika  jimbo hilo, Elias Ntiruhungwa amesema Kembaki amepata kura 18,235 huku Matiko  akipata kura 10,873. Ryoba Magwi wa ACT Wazalendo amepata kura 265 na Ester Nyagabona wa nccr-Mageuzi kura 143.

Korogwe mjini

Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Korogwe Mjini mkoani Tanga Nicodemus Bei amemtangaza Dk  Alfred Kimea (CCM) kuwa mshindi baada ya kupata kura 16,969,  Amina Magogo wa CUF kura 1,497, Winijonce Clarence wa Chadema kura 2,116 huku  Bahati Chirwa wa ACT- Wazalendo akipata kura 304.

Nzega Mjini

Hussein Bashe wa CCM amepata kura 16,082, Antony Sambali  wa ACT-Wazalendo 166, Andrew Atonga wa Chadema 2,663 na Masudi Salum wa CUF kura 102.

Endelea  kufuatilia Jamvi la Habari Digital  Kwa Taarifa Zaidi 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here