CCM: Asanteni Watanzania

0

NA MWANDISHI WETU

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM)  kimewashukuru Watanzania kwa kumchagua Rais John Pombe Magufuli Kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Dk Hussein Ali Mwinyi  kuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari jana  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,  Hamphrey Polepole alieleza kuwa Rais Magufuli na Mwenyekiti wa Chama hicho anawashukuru watanzania kwa kumteua kuwa Rais.

“Kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM na Mgombea Urais wa CCM na Rais Mteule John Pombe Magufuli  amewashukuru sana watanzania kwa kumchagua kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,”  alisema Polepole

Aidha ndugu polepole aliongeza kwa kusema kuwa leo siku ya Jumapili Rais Mteule Magufuli ataenda kuchukua hati ya uteule wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Kesho siku ya jumapili na kwa kadiri tutakavyoelekezwa na Tume ya Uchaguzi, Ndugu John Pombe Magufuli atapokea hati yake ya uteuzi kuwa rais mteule kule Dodoma, na hafla hiyo itakuwa na watu wachache sana” aliongeza Polepole

Polepole Pia alieleza kuwa siku ya Jumatatu Rais wa jamhuri ya muungan wa tanzania ataongoza shughuli ya kumuapisha rais Mteule wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi aliyechaguliwa na wananchi wa zanzibar kwenye uchaguzi wa Oktoba 28, 2020.

Polepole pia ameeleza kuwa mnamo siku ya Tarehe 5 Novemba mwaka huu Rais mteule wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Magufuli ataapishwa kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma.

“Siku ya terehe 5 mwezi wa 11 mwaka 2020, kutafanyika tukio kubwa la kihistoria la kumuapisha Rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli katika viwanja vya Jamhuri Dodoma,” aliongeza Polepole.

Aidha Polepole aliwaagiza wateule wote wa chama hicho kuanza maramoja kufanya tahmini na uchambuzi wa ahadi za chama hicho kwa Watanzania.

“Kuanzia leo hii wabunge wateule, wawakilishi wateule na madiwani wateule waanze kufanya uchambuzi wa ahadi zilizotolewa na wagombea urais wa Tanzania, Zanzibar pamoja na ilani ya ccm, na waanze kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua”-  aliongeza Polepole.

Aidha Polepole alieleza kuwa siri kubwa ya ushindi wa chama hicho kwenye uchaguizi wa mwaka huu ni mambo makubwa yaliyofanywa na chama hicho kikiongozwa na Rais Magufuli.

“Siri kubwa ya ushindi ni kazi iliyoongozwa na ndugu  magufuli
iliyoirudisha tanzania na kuifanya ing’ae kwenye ramani ya Dunia, Tanzania imevuka kutoka nchi maskini na kuwa nchi ya uchumi wa kati, sambamba na kuwa miongoni mwa nchi tatu zenye ukuaji mkubwa wa uchumi jumuishi” aliongeza Polepole

“Neno la ushauri kwa wapinzani, wakati mwingine kunapokuwa na agenda za kitaifa ni vizuri kushikamana pamoja, rais magufuli alivyona kwenye janga la korona aliagiza kumwomba mungu, huyu mungu yupo na anajibu, lakini mgombea wao hadharani walituita wajinga tukiomba” katibu huyo aliwashauri Viongozi wa Upinzani

Aidha Polepole aliwasihi Watanzania na Viongozi wa chama hicho waliopata nafasi kuwa katika awamu hii ya uongozi chama hicho kitasimamia kwelikweli utendaji na uwajibikaji wa wateule wake huku kikiahidi utumishi uliotukuka kwa wananchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here