Carlinhos akiri mambo yalikuwa magumu

0

NA MWANDISHI WETU

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Carlos Carlinhos, raia wa Angola, amekiri kuwa mwaka 2020 ulikuwa mzuri lakini hakuweza kufanya chochote kutokana na kuandamwa na wimbi la majeraha ya mara kwa mara tangu amejiunga na timu hiyo licha ya kupokelewa na mashabiki wengi.

Carlinhos alijiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Interclube ya Angola ambapo amefanikiwa kucheza mechi nne msimu huu huku akifunga mabao mawili na kutoa asisti mbili kabla ya kuanza kuandamwa na majeraha yaliyosababisha akae nje hadi sasa.

Carlinhos, alikiri kusumbuliwa na majeraha ya mfululizo kulimfanya ashindwe kutimiza majukumu yake ndani ya Yanga tangu amejiunga nayo mwanzoni mwa msimu huu.

“Kwanza kabisa namshukuru Mungu kwa kunibariki pamoja na familia yangu, ulikuwa mwaka mzuri kwangu, umeniathiri kwa majeraha ya mfululizo lakini bado nimekuwa na furaha katika mambo mengine.

“Naamini mwaka 2021 utakuwa mzuri na wenye mafanikio mengi kwa kuhakikisha kila mmoja anapigania malengo yake,”alisema Carlinhos.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here