BREAKING NEWS: MAJALIWA AFUNGUKA AFYA YA RAIS MAGUFULI

0

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka watanzania kuwapuuza wapotoshaji wanaosambaza taarifa za chuki, uongo na kuzua taharuki miongoni mwa wanajamii kuhusiana na afya ya Rais John Pombe Magufuli.

Akizungumza baada ya Swala ya Ijumaa katika Msikiti Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Waziri Mkuu Majaliwa amesisitiza kuwa tabia ya watanzania wenzetu wanaoishi nje ya nchi ya kupotosha makusudi mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya nchi pamoja na Kuzusha Uongo

“kwa hili na mimi Nionyeshe Masikitiko yangu kwa wanaosambaza uzushi juu ya afya ya Kiongozi wetu na kuleta taharuki kuwa rais wetu anaumwa jambo ambalo ni uongo kwani mimi asubuhi nilizungumza naye nikamfahamisha juu ya ziara yangu mkoani Ruvuma” Aliongeza Waziri Mkuu Majaliwa

“Rais ana Mambo Mengi na Kutoka kwake ni kwa ratiba ya mpango kazi wake, unataka rais atoke aanze kuzurura Kariakoo, au aanze kuzurura Magomeni, au unataka azunguke kwa ratiba yako?” Aliongeza Majaliwa

Aidha Waziri Mkuu Majaliwa amewataka watanzania Kuwaombea Viongozi wakuu wa nchi kwani wana Dhamana kubwa ambayo wamepewa na Watanzania ya kuwatumikia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here