Bonnah Kamoli atetea jimbo lake la Segerea

0

Mwandishi Wetu 

Mbunge aliyekuwa anatetea kiti chake katika Jimbo la Segerea kutoka CCM, Bona Kamoli ametangazwa kushinda baada ya kumshinda mpinzani wake, John Mrema wa Chadema kwa kura 76,828 sawa na asilimia 65.8.

Akitangaza matokeo ya jimbo hilo asubuhi hii ya Ijumaa Oktoba 30, 2020, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Jumanne Shauri amesema mgombea wa Chadema amepata kura 27,612 sawa na asilimia 23.6.

Mgombea kupitia ACT Wazalendo Mbarala Maharagande amepata kura 4,454, Sabreena Hamza wa CUF kura 3,649 na  Zawadi Mohammed AAFP kura 614.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here