
NA MWANDISHI WETU
PROMOTA wa mchezo wa masumbwi nchni Rajabu Mhamila ‘Super D’ amemsainisha bondia Hamisi Maya kwa ajili ya kuzipiga na Ahmed Hendy kutoka Egyty mpambano wa raundi nane utakaofanyika katika ukumbi wa Saba Saba Hall uliopo katika viwanja vya maonesha vya Sabasaba (PTA), jijini Dar es Salaam.
Pambano hilo, lilitakalowakutanisha wababe hao, linatarajiwa kupigwa Februari 14 mwaka huu, jijini Dar es Salaam
Akizungumza mara baada ya kutiliana saini katika mkataba wa kuzipiga Promota Super ‘D’ alisema kuwa Maya ni bondia bora mchini ambapo mwaka jana alinyakuwa ubingwa wa Mabara wa GBC, nchini Ujerumani.
“Alifanikiwa kurudi na ubingwa huo hata hivyo mpaka sasa ajautetea hivyo kampuni ya kizalendo ya Super ‘D’ Boxing Promotion tumeamua sasa kumuinua kwa kumuandalia mpambano wa kimataifa hapa hapa nyumbani ili aoneshe uwezo wake na kipaji alicho nacho,”alisema Super ‘D’.
Naye Maya, aliishukuru Kampuni ya Super ‘D’ Boxing Promotion kumsainisha kwa ajili ya mpambano wake mwingine wa kimataifa utakaofanyika hapa nchini.
“Hivyo naomba mashabiki wangu waje kwa wingi ili niwaoneshe radha ya mchezo wa masumbwi walio ikosa kwa muda mrefu sasa nitacheza kwa kujivunia kwa kuwa nitakuwa katika uwanja wa nyumbambani,”alisema Maya