Boko Haram yawaachilia huru Wanafunzi 344

0

Mamia ya wavulana waliotekwa wiki iliyopita kutoka shule ya bweni kaskazini -magharibi mwa Nigeria wameachiliwa huru, mamlaka katika eneo hilo zimeambia BBC.

Msemaji wa gavana wa jimbo la Katsina amesema wavulana 344 wameachiliwa huru na kwamba wako katika hali nzuri.

Hata hivyo, ripoti zingine zinaashiria kuwa baadhi yao wamesalia mikononi mwa watekaji wao.

‘Jinsi nilivyotoroka watekaji’ – mwanafunzi Nigeria
Shambulio hilo linadaiwa kutekelezwa na na wanamgambo la Boko Haram, ambalo awali lilitoa video ikiwaonyesha baadhi ya wavulana hao.

Katika taarifa yake, msemaji, Abdul Labaran, amesema wavulana hao walikuwa wakipelekwa katika mji mkuu wa mkoa wa Katsina, na hivi karibuni wataungana na familia zao.

Amesema video iliyotolewa na na Boko Haram ilikuwa ya kweli, lakini ujumbe unaonekana kutoka kwa kiongozi wa kikundi hicho Abubakar Shekau, ulikuwa wa kuiga.

Hapo awali mamlaka zilitoa idadi ndogo kuliko ile yiliyotolewa na wenyeji kama jumla ya vijana waliotekwa nyara na hadi sasa haijulikani ikiwa wote wako salama.

Gavana wa jimbo hilo Aminu Bello Masari alinukuliwa na shirika la habari la Reuters akisema, “tumepata wavulana wengi. Sio wote,” huku chanzo cha usalama kililiambia shirika la habari la AFP wengine walibaki na watekaji wao.

Bwana Labaran alisema hakuna hata mmoja wa wavulana waliotekwa nyara aliuawa, huku maoni yake yakikinzana nay ale ya mvulana aliyeonyeshwa kwenye video hiyo ambaye alisema kuwa wengine waliuawa na ndege za kivita za Nigeria

Haijulikani jinsi kuachiliwa huru kwa wavulana hao kulitokea lakini habari hiyo imethibitishwa kwa BBC Hausa na afisa mwingine wa serikali ya jimbo hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here