Boko Haram yashambulia vijiji mkesha wa Krismasi

0

LAGOS,NIGERIA

WATU  kadhaa wameuawa Kaskazini Mashariki mwa Nigeria baada ya wanamgambo wa Boko Haram kushambulia vijiji vya Wakristo na kuteketeza Kanisa mkesha wa Krismasi.

Vyanzo vya habari katika eneo hilo vinasema karibu watu wa 11 wameuawa, kulingana na shirika la habari la AFP.

Wapiganaji waliingia Pemi katika jimbo la Borno, kwa kutumia magari na piki piki na kuanza kufyatua risasi kiholela, mmoja wa viongozi katika kijiji hicho aliambia shirika hilo la habari.

Pemi iko karibu na Chibok ambako wasichana 200 wa shule walitekwa mwaka 2014.

Boko Haram wamefanya mashambulio kadhaa kaskazini mwa Nigeria ambako wanapigana kupindua serikali ili kubuni taifa la Kiislamu.

Siku ya Alhamisi, wapiganaji walivamia Pemi kama walivyokuwa wameonya maafisa wa usalama huenda kukatokea mashambulio hasa wakati wa Siku kuu ya Wakristo

Wanavijiji walitorokea msituni na baadhi yao bado hawajulikani waliko.

“Magaidi waliwaua watu saba, kuchoma moto nyumba 10 na kuiba bidhaa za chakula ambazo zilikuwa zigawanyiwe wakaazi wakati wa sherehe ya Krismasi ,”kiongozi wa wanamgambo Abwaku Kabu alisema.

Wasambuliaji walichoma moto kanisa, kumteka mchungaji na kuiba bidhaa za matibabu katika hospitali moja kabla ya kuiteketeza moto.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here