Biteko ashtukia ukiukwaji Sheria mgodi wa North Mara

0
Waziri wa Madini Doto Biteko katikati akimsikiliza Mameneja wa Mgodi wa North Mara Hilaire Diarra akitoa maelezo kuhusu uhifadhi wa tope sumu (TFS), mwenye shati la Kijani ni Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima, kushoto kwa waziri ni Mkurugenzi wa Migodi kutoka Tume ya Madini Dk. Mwanga, na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu Rais Muungano na Mazingira, Mwita Waitara.

Na MWANDISHI WETU, MARA

Imeelezwa kwamba mgodi wa North Mara umekiuka Sheria ya Ushirikishwaji wa Watanzania (local content) baada ya kutangaza zabuni nje ya nchi na kupata mzabuni kinyume  cha Sheria za Madini.

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Madini Doto Biteko baada ya kufanya ziara maalum mgodini hapo Desemba 18, 2020.

Kanuni za Madini (Ushirikishaji wa Watanzania), 2018 Tangazo la Serikali Na. 2/2018 zinataka wamiliki wa migodi kutangaza zabuni hapahapa nchini na endapo hakuna mtanzania mwenyewe sifa au vinginevyo, zabuni hiyo inatangazwa nje ya nchi na atakaepatikana atalazimika kushirikiana na Mtanzania.

Biteko alisema, kwa mujibu wa sheria hiyo, mgodi utakaokiuka utatozwa adhabu ya dola za kimarekani milioni tano.

Aliongeza kuwa sheria hiyo inalenga kutoa fursa ya watanzania katika kushiriki masuala ya uchumi wa madini.

Meneja Mkazi wa Mgodi wa North Mara, Hilaire Diarra, alikiri kosa la kutofuata sheria kwa kuwa walikuwa katika presha ya kutekeleza mradi huo. Diarra aliomba radhi na kwamba wapo teyari kufuata maelekezo yatakayotolewa na Serikali.

Kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeo ya jamii (CSR), Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila alihoji kuhusu utekelezaji wa (CSR). Meneja Mgodi anaeshughulikia Mahusino Gilbert alisema wametekeleza kwa kujenga madarasa, kujenga visima vya maji na masuala ya afya japo Prof. Msanjila alimwambia hawajafuata utaratibu unaotakiwa katika kutekeleza miradi ya CSR.

Kutokana na majibu hayo, Biteko aliuagiza wa mgodi huo kuanda mpango wa utekelezaji wa miradi ya CSR na kuwasilisha kwenye mamlaka ya serikali za mitaa ili waipitie na kuidhinishwa teyari kwa ajili ya kutekeleza.

Akizungumzia kuhusu masuala ya fidia, Biteko amesema wanaolipwa ni wale wenye haki akisisitiza kuwa utaratibu wa mtindo wa watu ku tegesha hawawezi kulipwa fidia.

Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, amesema suala la fidia nyamongo linacheleweshwa na wananchi kutokwa na mchezo wa suala ya tegesha. Amesema watu watakao bainika sheria itachukuwa mkondo wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here