Biteko acharuka utoroshaji madini Chunya

0

Na Mwandishi Wetu 

Waziri wa Madini Doto Biteko amefuta leseni Sita za wafanyabiashara wa madini ya dhahabu ambao wanatuhumiwa kujishughulisha na utoroshaji wa madini wilayani  mkoani Mbeya.

Pia ameagiza Mawakala wa Wanunuzi wa Dhahabu 13 kukamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na utoroshaji madini, watuhumiwa wote hao, wametakiwa kutojishughulisha na shughuli yoyote ya Madini nchini.

Wakati huo huo, Waziri Biteko, ameagiza kuondolewa kwa Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa Madini ya dhahabu anaye husika na usimamizi wa Soko la Madini la Chunya, Gagala Poul.

Biteko amechukua hatua hizo leo disemba 14, 2020 kwenye mkutano wa wachimbaji wadogo wa dhahabu na wadau wa madini wilayani Chunya.

Katika hatua nyingine Waziri Biteko amewasimamisha kazi watumishi watatu wa Ofisi ya Madini wa Mkoa wa kimadini wa Chunya baada ya kutuhumiwa kushirikiana na wafanyabiashara kutorosha madini, ambao watumishi hao ni Gabliel Masai, Edward Gavana na George Wandiga.

Pia, Waziri Biteko, ameagiza kusajiliwa kwa Mialo yate inayo chenjua madini ya dhahabu wilayani Chunya ili kujua mwalo gani umezalisha kiasi gani cha dhahabu na dhahabu hiyo imepelekwa kuuzwa soko gani.

“Bora tubaki na wanunuzi wawili wa madini ya dhahabu ambao ni waanifu kuliko kuwa na mlolongo wa wanunuzi ambao sio waaminifu na wasio fuata kanuni, taratibu na sheria zilizowekwa,” amesema Biteko.

Waziri Biteko amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila kutoa zawadi wale wote watakao saidia kupatikana kwa watu wanao torosha madini.

“Niwaombe wachimbaji na wafanyabiashara wote wa madini kutoa ushirikiano kwa Serikali ili kukomesha tatizo la utoroshaji madini, tunataka nidhamu kwenye sekta ya madini ili tulete tija na maendeleo nchini,” amesema Waziri Biteko.

Pia, Waziri Biteko, amewataka wachimbaji na wafanyabiashara wote wa madini nchini kuhakikisha wanapeleka madini yao sokoni na kuachana na ufanyaji biiashara ya madini nje ya masoko ya madini.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema suala la utoroshaji madini ni aibu na fedhea kwa viongozi wa mkoa.

Chalamila amesema utoroshaji huo wa madini umewadhalilisha viongozi na walipaswa kujipeleka polisi ili wahukumiwe walau miezi sita jela.

“Kimsingi, mkoa na viongozi tumedhalilika sana. Tulipaswa kujipeleka wenyewe polisi na si vinginevyo,” amesema.

Pia, Chalamila amesema tayari Serikali imeanza kujenga gereza ili watu watakao kamatwa wakitorosha madini hawatapekwa mbeya mjini bali watafungwa katika gereza hilo.

MCHANGO WA SEKTA YA MADINI KIUCHUMI

Tangu kuingia kwa Serikali ya awamu ya tano Mapato ya sekta ya madini yameongezeka kutoka Sh. bilioni 168 mwaka 2014/2015 hadi Sh.  bilioni 527 mwaka 2019/2020.

Mchango wa sekta ya madini kwenye Pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 3.4 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 5.2 mwaka 2019. Zaidi ya hapo, kwa mara ya kwanza, katika historia ya    Tanzania, mwaka 2019, sekta ya madini iliongoza kwa kuingiza fedha nyingi za kigeni, kiasi cha Dola za Marekani bilioni 2.7.

Hata hivyo katika hotuba yake ya kufungau Bunge la 12 Rais Dk. John Magufuli alisema anataka katika miaka mitano ijayo sekta ya madini ichagnie asilimia 10 ya pato la Taifa na kuanisha hatua mbalimbali zitakazochukuliwa ikiwemo kuendelea kudhibiti utorishaji wa madini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here