Biden ashinda urais Marekani

0

NEW YORK, Marekani

Joe Biden ametangazwa kuwa mshindi wa Urais nchini Marekani na amekuwa rais mteule wa wa taifa hilo.

Jana, asubuhi Biden alisema anaamini anakaribia kushinda kwenye uchaguzi huyo na kumshinda Rais Donald Trump.

Mgombea huyo wa chama cha Democrat sasa ana kura 253 kati ya 270 za wajumbe zinazohitajika chini ya mfumo wa kura za majimbo ili kukalia Ikulu ya Marekani.

Biden anaongoza kwa kura katika majimbo muhimu ya Georgia, Nevada, Pennsylvania na Arizona.

Ushindi wa Biden utamfanya Trump kuondoka madarakani mwezi Januari baada ya kuwa madarakani kwa miaka minne.

“Tunakwenda kushinda kinyang’anyiro hiki,” Biden amewaambia wafuasi wake mjini Wilmington, Delaware,usiku wa Ijumaa, akieleza kwa sauti ya kujiamini. Akiwa sambamba na mgombea mwenza, Seneta wa California Kamala Harris.

Alisema kuwa yuko njiani kupata kura zaidi ya 300 na kubainisha kuwa watu wengi zaidi wamempigia kura- zaidi ya watu milioni 74 – kuliko mgombea mwingine yoyote wa urais katika historia ya Marekani.

Biden alisema Wamarekani wamempa mamlaka ya kupambana na janga la virusi vya corona, uchumi unaoyumba, mabadiliko ya tabia nchi na ubaguzi wa rangi. Siku ya Ijumaa ikiwa siku ya tatu mfululizo Marekani imerekodi maambukizi ya watu 127,000 kutokana na virusi vya corona.

“Tunaweza kuwa wapinzani lakini sisi si maadui, sisi ni Wamarekani,” alisema Biden, ambaye hakumtaja mpinzani wake wa Republican.

Kuonekana kwa Bwana Biden hapo awali kulikuwa kumepangwa kama hotuba ya ushindi, lakini aliamua badala yake kutoa taarifa ya jumla juu ya hali ya mchakato huu wakati mitandao ya Runinga ya Marekani ikiwa makini kutomtangaza kuwa mshindi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here