Biashara haramu ya watoto inavyotikisa Kenya

0

NAIROBI,KENYA

HIVI karibuni, Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) lilifichua biashara haramu ya watoto katika jiji la Nairobi nchini Kenya.

Kutokana taarifa hiyo, polisi waliwakamata watu saba kwa makosa ya uuzaji na usafirishaji wa watu. Je, nini kinamsukuma mama kuuza mtoto wake? Fuatilia.

 Maisha ya Adama yalikuwa mazuri wakati alipokuwa akiishi na wazazi wake. Alipelekewa shule, akaipenda sana.

Lakini baba yake alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 12, na kasha mama yake pia akafariki dunia miaka michache baadaye.

 “Maisha yalibadilika yakawa magumu sana,” anasema katika mazungumzo akiwa kijijini anakoishi, mashariki mwa Kenya.

 “Nililazimika kuacha shule na kuanza kujitegemea.” Akiwa na miaka 22, Adama alikutana na mwanaume mmoja aliyempa ujauzito.

Lakini mwanaume huyo alikufa siku tatu baada ya mtoto wao wa kike kuzaliwa. Alijikuta mpweke na kumnyonyesha mwanae kwa shida sana.

Akiwa na mezi 18 aliamua kumwacha mtoto wake kwa bibi yake na kwenda kutafuta maisha jijini Nairobi.

 “Kumbuka kuwa umeacha mtoto jitahidi ulete matunzo kwa mtoto,” bibi yake alimwambia wakati anadoka.

 Adama alipofika Nairobi, alianza kwa kuuza matikiti maji barabarani. Licha ya kupata pesa kidogo na kujiwekea akiba, mtu aliyekuwa akiishi naye alimwibia fedha aliyoiacha nyumbani na kutoweka.

 “Maisha katika jiji yalikuwa magumu zaidi baada ya hapo,”anasema Adama.

Alipata kibarua cha ujenzi lakini hakulipwa kabisa, na alipotoka hapo akaamua kwenda kwenye kilabu cha usiku alikokuwa bosi wake na kumtaka malipo yake amtumie bibi yake kijijini moja kwa moja.

Baada ya muda, Adama alipata mshahara uliomsaidia kidogo kuishi katika jiji la Nairobi na kupanga chumba baada ya kupata kibarua kingine kwenye kampuni la ujenzi.

Katika kipindi hicho alikutana na mwanaume mmoja ambaye walianza kuwa na urafiti wa kimapenzi na kasha mwanaume huyo akamwambia kwamba alikuwa anataka kupata mtoto na yeye Adamu alimpa masharti kwamba kama anataka kumzalia mtoto, basi awe tayati kumleta mtoto wake wa kike aliyemwacha kijijini waishi waishi wote Mwanaume huyo akakubali.

Anasema katika kipindi cha miezi mitano ya ujauzito, mwanaume huyo alilipa kodi ya nyumba na Adama akawa anasubiri muda mwafaka wa kumleta mtoto wake wa kike jijini.

Siku moja yule mwanaume aliondoka lakini hakurudi tena hadi leo. Ni katika mazingira kama hayo ya Adama inaelezwa kwamba baadhi ya akina mama jijiji Nairobi wanalazimika kuuza watoto wao ili waweze kuishi kwani hali inakuwa mbaya sana kwao.

Lakini malipo wanayopewa ni kiasi kidogo sana. Binti mwingine, Sarah, alikuwa na umri wa miaka 17 pale alipojikuta akiwa na ujazito wa pili huku akiwa hana uwezo wowote wa kumwezesha kulea mtoto. Akaamua kumuuza kwa mwanamke ambaye alikuwa tayari kumnunua kwa shilini 3,000 za Kenya (Sh 62,000 za Tanzania).

 “Wakati huo nilikuwa bado mdogo. Sikufikiria kama nilichokuwa ninafanya ni kosa,” anasema. “Baada ya miaka mitano nilianza kujisikia vibaya na kumtaka mwanangu na nilitaka nirudushe fedha,” anasema na kuongeza kwamba wakati anamuuza mwanae alikuwa pia akimjua mwanamke mwingine ambaye pia aliuza mwanae.

“Wasichana wengi huuza watoto wao kwa sababu ya changamoto za maisha. Anaweza akawa amefukuzwa nyumbani na wazazi wake baada ya kupata mimba na hana kitu, au alikuwa bado shuleni wakati alipopata ujauzito.

 Hiyo ni shida kubwa kwa msichana ambaye ana miaka 15 au 16. “Utakuta wasichana Nairobi wanapoteza watoto wao na kila kitu wanachomiliki kwa sababu hakuna mtu wa kuwashika mkono wanapokuwa kwenye changamoto kubwa za maisha.

” Kenya inatajwa kuwa moja ya nchi yenye viwango vya juu zaidi vya mimba za utotoni barani Afrika, na wataalamu wa afya wanasema tatizo limekuwa baya zaidi wakati huu wa janga la corona huku baadhi ya wanawake wakilazimia kujiuza ili mkono upate kwenda kinywani.

“Nimesikia hadithi nyingi za wanawake na wasichana katika hali hii. Wasichana wadogo wanakuja katika miji kutafuta kazi, wanaingia kwenye mahusiano, wanashika mimba na kutelekezwa na waliowapa mimba,” Prudence Mutiso, mwanasheria wa haki za binadamu nchini Kenya anasema.

“Baba anapokimbia majukumu, huyu msichana anajikuta akilazimika kutafuta njia nyingine ya kuishi. Na hayo ndiyo yanayowasukuma wasichana kuuza hawa wa watoto, ili waweze kupata kipato cha kujikimu na wemngine kusaidia malezi ya watoto wao ambao tayari wamewaacha vijijini kwao. Watu hawazungumzi juu ya hili wazi, lakini lipo.

 ” Adama alificha ujauzito wake kwa muda mrefu alipokuwa kwenye kampuni la ujenzi, hadi ilipofikia hatua kwamba hawezi tena kubeba mfuko mzito wa saruji.

 Tumbo pia lilikuwa linazidi kuwa kubwa. Baada kushindwa kazi hakuwa na mapato ya kulipia kodi ya pango. Kwa miezi mitatu, mwenye nyumba alimvumilia, kisha akamfukuza na kupangisha hicho chumba mtu mwingine.

Katika ujauzito wa miezi nane, Adama alijikuta akilazimika kulala usiku sana na kuondoka asubuhi na mapema.

 “Kuna siku ningebahatika kupata chakula lakini wakati mwingine nilikuwa nikinywa maji tu, nasali na kulala.” Nchini Kenya, kutoa mimba ni kosa la jinai labda kama mama wa motto atakuwa katika hatari ya kupoteza maisha na hakuna elimu yakutosha inayotolewa kwa wasichana kuhusu elimu ya uzazi salama na hatari ya kuzaa katika umri mdogo.

“Wasichana wanaopata mimba zisizotarajiwa hawapati msaada wowote kutoka kwa serikali,” anasema Ibrahim Ali, meneja programu wa asasi ya kiraia iitwayo Health Poverty Action.

Tukirudi kwa Adama anasema alikuwa hajui taratibu za kisheria za kumpa mtu aliye tayari kumwasili mwanae na wala alikuwa hajawahi kusikia kitu kama hicho.

Anasema kuna wakati alifikia hatua ya kutaka kutoa mimba baada ya bwana aliyempa mimba hiyo kutoweka lakini akahofia maisha yake kwani mimba ilishakuwa kubwa.

“Nilikuwa na msongo wa mawazo, nilianza kufikiria ni jinsi gani ningejiua ili niondokane na adha za maisha ya dunia na watu wanisahau,” anasema.

 Lakini wiki chache kabla ya tarehe yake ya kujifungua, mtu mmoja alimtambulisha Adama kwa mwanamke aliyevalia vizuri anayeitwa Mary Auma, ambaye alimwambia asitoe mimba au kujiua.

Auma aliendesha kliniki ambayo haijasajiliwa katika mtaa wa Kayole jijini Nairobi. Alimpatia Adamu shilingi 100 (Sh 2,061) na kumwambia aendele kwenye kliniki yake siku iliyokuwa inafuata.

Kliniki ya Mary Auma wala si kliniki bali vyumba viwili vilivyo mafichoni katika Mtaa wa Kayole ambako wasichana kama Adama hujifugulia.

 Mwanamke huyo alimwambia kwamba kuna wazazi wamekosa mtoto ambao walikuwa tayari kumnunua mwanae lakini ukweli ni kwamba Auma alikuwa anajipanga kuuza mtoto wa Adama kwa yeyote mwenye pesa ndefu.

Mwanamke huyo anadai ana taaluma ya uuguzi na kwamba alikuwa kufanya kazi ya uuguzi kwenye hospitali kubwa lakini hana nyataraka kuthibitisha madai hayo.

Uchunguzi wa BBC uligundua kwamba chumba chake amacho wasichana wanajifungulia ni kichafu, wala vifaa maluumu kwa ajili hiyo hakuna.

 Adama alipofika kwenye kliniki, Mary Auma alimpa vidonge viwili bila maelekezo ili kusabaisha uchungu kuja haraka, anasema Adama na kwamba mnunuzi wa mwanae alikuwa tayari amepangwa.

 Lakini wakati Adama alipojifungua mtoto wa kiume alipata shida ya kifua na hivyo alihitaji huduma ya haraka, na Auma akamwambia Adama ampeleke hospitalini.

Baada ya wiki akiwa amelazwa hospitali, Adama aliruhusiwa kuondoka na mwanae na hapo ndipo Auma alianza kutafuta dili la kuuza mtoto huyo.

Mmoja wa watu waliojotokeza kununua mtoto wa Adama ni mwandishi wa BBC aliyekuwa anafuatilia mpango mzima na alijifanya kuwa tayari kulipa Sh 45,000 za Kenya au Sh 927,706 za Tanzania lakini Auma angempa Adama Sh 206,157 (Sh 10,000 za Kenya).

Adama alikabidhi mwanae wa kiume katika kituo cha serikali cha kuelelea watoto wenye matatizo ambako anatunzwa hadi atakapopapata mtu wa kumwasili.

BBC alimtaka Mary Auma kujibu tuhuma zake kuhsu sakata hili lakini amegoma kuzungumza. Adama akiwa na umri wa miaka 29 sasa amerudi kijiji kwao alikolelewa.

Maisha hayajabadilika sana kwani anaishi kwa kutegemea vibarua na kuna siku anakwenda kulala bila kutia kitu tumboni. Ana ndoto za kufungua duka la viatu kijijini kwao akivitoa Nairobi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here