Beyonce, Rihanna na TaylorSwift Vinara wanawake wenye ushawishi mkubwa duniani

0

WASHINGTON, MAREKANI

KILA mwaka Jarida maarufu ‘Forbes’ hutoa orodha ya wanawake 100 wenye nguvu na ushawishi zaidi Duniani hivyo basi kati ya wasanii wengi wakike Duniani, wanamuziki hawa watatu tokea nchini Marekani yaani Beyonce, Rihanna na TaylorSwift wamepita kwenye orodha hii ya mwaka 2020.

Katika orodha hiyo warembo hao wameng’ara kwa kukamata nafasi mbalimbali, ambapo Rihanna kashika nafasi ya 69 huku Beyonce akishika nafasi ya 72 na Taylor Swift akikaa kwenye nafasi ya 79.

Miongoni mwa vitu vilivyo wapandisha wasanii hao ni pamoja na kujitolea kwenye jamii hasa kipindi hiki cha mlipuko wa janga la virusi vya Corona.

Wapo wengine wengi pia kama vile Queen Elizabeth II, Oprah Winfrey, Kamala Harris (Makamu wa Rais Marekani), Ava Duvernay na mwanasiasa Stacey Abraham huku mwanamama kiongozi Angel Merkel akiwa juu yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here