Ben Pol kuufunga mwaka 2020 kwa ‘style’ ya kipekee

0

NA MWANDISHI WETU

MSANII wa Muziki wa Kizazi kipya Bongo Fleva, Ben Pol anatarajia kuuaga mwaka 2020 na kuukaribisha mwaka 2021 kwa staili ya kipekee.

Ben Pol anatarajia kufanya show kubwa ya Muziki wa Live na chakula cha jioni pamoja na mashabiki wake.

Show hiyo inatarajiwa kufanyika Ramada Hotel, Mbezi Beach Dar es Salaam katika mkesha wa mwaka mpya yani leo (31.12.2020) ambapo ataanza kwa kujumuika katika chakula cha jioni pamoja na mashabiki zake watakaohudhuria usiku huo.

Ben Pol alisema, pia kutakuwa na michezo ya watoto, urushaji wa fataki pamoja na muziki wa live ukiongozwa na Ben Pol na bendi yake.

“Mashabiki zangu wamekuwa wakizipokea vizuri sana kazi zangu kwa zaidi ya miaka 10 sasa, Nashukuru kwa upendo na support kubwa wanayonipa, nina kila sababu ya kusherehekea kwa kujumuika nao kwa chakula na muziki mzuri wa live kwenye mkesha wa mwaka mpya, na hii haitoishia hapa.

“Nitazunguka mikoani kufanya kitu kama hiki naomba nao pia wajiandae kunipokea tukijaaliwa uzima,”alisema Ben Pol.

Ben Pol kwa sasa anatamba na Wimbo wa Kidani aliomshirikisha mkewe Anerlisa kwenye video.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here