Beki aliyemkaba Messi Afrika Kusini afariki dunia

0

JOHANNESBURG, AFRIKA KUSINI

BEKI wa Mamelodi Sundowns Motjeka Madisha, amefariki akiwa na miaka 25. Taarifa zimeeleza kuwa Madisha amefariki kwenye ajali ya gari alfajiri ya jana, Desemba 13, 2020 huko Johannesburg.

Madisha ameichezea Mamelodi zaidi ya mechi 130 na kushinda makombe matatu ya ligi kuu pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika na Super Cup.

Beki huyo ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa tegemeo kwenye mafanikio ya Mamelodi chini ya kocha Pitso Mosimane, ambapo mbali na ligi pamoja na klabu bingwa pia walishinda mataji mbalimbali kama Telkom Knockout, the Nedbank Cup.

Pia nyota huyo ameichezea timu ya taifa ya Afrika Kusini akijihakikishia nafasi kwa miaka ya hivi karibuni.

Motjeka Madisha pia alimkaba Lionel Messi kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa Mei 16, 2018 na kumalizika kwa Barcelona kushinda magoli 3-1.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here