Home BURUDANI BASATA yakabidhiwa rasimu mpya ya katiba kuwaongoza wasanii

BASATA yakabidhiwa rasimu mpya ya katiba kuwaongoza wasanii

NA REHEMA KIVUMBI

Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) limekabidhi rasimu ya Katiba mpya kwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambayo imechukua takribani mwaka mmoja kukamilika kwake baada ya kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali ambapo imelenga kutatua migogoro kwenye tasnia ya filamu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Februari 26, baada ya kukabidhi rasim hiyo, Rais wa Shirikisho hilo, Simon Mwakifamba, amesema Katiba mpya itapunguza migogoro ambayo imekuwa ikirudisha nyuma maendeleo ya filamu kutokana na baadhi ya viongozi kutowajibika.

“Nimekabidhi Rasimu hii kwa ajili ya wasanii kuzingatia sheria zinazohusiana na filamu, kwa mfano zamani tulikuwa tunaona wasanii wa muziki wanahamia kwenye uigizaji wa filamu pasipo kufuata utaratibu maalumu, hawafuati maadili yetu ya Kitanzania kwa sababu walikuwa hawana sheria zilizokuwa zikiwabana lakini Rasimu hii itasaidia kuwarudisha wasanii katika utaratibu maalum”.

“Kwa Rasimu hii wasanii wataacha kuilaumu Serikali kwa sababu hapo awali watu walikuwa wanaibuka na kuanzisha vikundi vya filamu bila kufuata utaratibu maalum, wanatoa filamu zenye ubora wa kiwango cha chini wanakosa soko wanaanza kurusha lawama kwa Serikali, sasa Serikali hii itasaidia watu wangapi hivyo nawaomba wasanii kwa sasa mfuate sheria zilizopo kwenye Rasim hii,”- amesema Mwakifamba.

Aidha Mwakifamba ameongeza kuwa Rasimu ya katiba mpya itawasaidia wasanii kuzalisha filamu zenye ubora pamoja na kulinda maslahi ya wasanii ambapo kuna kundi kubwa la watu watakaofaidika kutokana na katiba hiyo mpya.

Kwa upande wa Mwanasheria wa BASATA, Onesmo Ndinga amesema wameipokea Rasim hiyo na wataipitia kuona iwapo vipengele vilivyokusudiwa kurekebishwa vimefanyiwa kazi na wamezingatia maslahi ya msanii, kuzalisha filamu bora na msanii kufuata utaratibu na maadili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -

Most Popular

Yanga yampatia Tshishimbi mkataba mpya

NA MWANDISHI WETU Klabu ya Yanga SC, imesema kuwa tayari imemaliza kazi yake ya kuhakikisha inambakiza kiungo tegemeo wa...

Tetesi za soka barani Ulaya

SANCHO AITIKISA UNITED Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Timu ya Taifa ya Uingereza, Jadon Sancho (20), amesema hatakuwa tayari...

Makonda: Wazururaji hawatakwenda mahabusu watazibua mitaro ya maji machafu

NA MWANDISHI WETU Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kuwa watu watakaokamatwa kwenye mkoa huo kutokana...

Chui katika hifadhi ya wanyama ya Bronx akutwa na Virusi vya Corona

NEW YORK, MAREKANI Chui wa kike wa Malaysia aliyefahamika kwa jina la Nadia mwenye umri wa miaka minne katika hifadhi...

Recent Comments