BASATA: Vyama vijipange kwa uchaguzi

0

NA MWANDISHI WETU

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limetoa wito kwa viongozi  wa vyama vya Sanaa ya muziki kujipanga vilivyo kwa ajili ya uchaguzi unaotarajia kufanyika mapema mwakani.

Akizingumza katika mkutano maalum kwa waimbaji wa nyimbo za injili na wa miondoko mingine uliofanyika jana, Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza, alisema wanamuziki wanatakiwa kuzingatia suala la utawala bora ili kutekeleza majukumu yao inavyotakiwa.

Mkutano huo, maalum ulikuwa ni maalum kwa zoezi la ugawaji wa kadi za Bima ya Afya kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ambako wanachama 45 walipatiwa kadi zao.

Mngereza alisema wanatarajia zoezi la uchaguzi litakamilika hadi mwishoni mwa Januari 2021.

Mngereza, alisema waimbaji wa nyimbo za injili wanabeba dhamana kubwa kwa jamii ikiwemo ya kibinaadam na kimungu na kueleza kwamba waimbaji wamepewa maono makubwa na Mungu.

Aidha, Mngereza alitumia fursa hiyo kueleza kwamba kwa kuwa teknolojia imekuwa anatamani ungepatikana mfumo maalun wa udhibiti wa wizi kama ilivyofanywa kwenye magari na sehemu nyenginezo.

Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Ado Novemba alitoa pendekezo kwamba baada ya uchaguzi, viongozi watakaopatikana wataapishwa kwa taratibu za kisheria.

Novemba alisema kwamba wajitokeze wagombea wenye maono ya kusaidia muziki kupiga hatua stahili.

Novemba alisema wanamuziki wanarakiwa kurudisha ari ya awali ambayo ilichochea ushirikiano wa hali ya juu na utekelezaji wa majukumu ya chama hicho.

Baadhi ya waimbaji mahiri waliofika katika matukio hayo ni John Kitime, Mjusi Shemboza, Jesca Honore, Jennifer Mgendi, Emmanuel Mabisa, Ambwene Mwasongwe, Bahati Bukuku na wengineo wengi.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here