Barnaba:Kiki hazijawahi kuinua mziki

0

NA MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM

UNAPOWAZUNGUMZIA wanamuziki wenye tungo nzuri na wanaojua kutumia vyombo vya muziki Bongo, kamwe huwezi kulitaja jina la kijana ambaye aliibuliwa kipaji chake na aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, Barnaba Elias.

Mwanamuziki huyu, hivi karibuni ilisemekana anaumwa sana na ndiyo sababu iliyomfanya asisikike kwa muda kidogo.

Amani Vibes imemsaka na kufanikiwa kuzungumza naye ambapo amesema amesekia tetesi hizo za yeye kuumwa lakini ukweli ni kwamba yuko vizuri na hana tatizo lolote.

Akizungumza na moja ya chombo cha habari nchini Barnaba anasema pamoja na ukimya wake uliopo sasa lakini hana tatizo lolote.

Mwandish: Barnaba habari za siku?

Barnaba: Nzuri kabisa, vipi hali?

Mwandishi : Salama, Barnaba umekuwa kimya sana kwa sasa nini tatizo?

Barnaba: Hapana sina shida yoyote ile maana muziki ni kujipanga na sio kukurupuka kabisa.

Mwandishi: Kuna tetesi kwamba unaumwa?

Barnaba: (kwa mshangao) Ninaumwa nini mimi mbona sina tatizo lolote lile.

Mwandishi: Kuna habari kuwa umepata tatizo la koo kama ilivyokuwa kwa Ommy Dimpoz?

Barnaba: Hakuna kitu kama hicho na ninaomba Mungu azidi kunisimamia maana kukaa kimya sio kwamba naumwa au nina tatizo lolote bali najipanga zaidi.

Mwandushi:Maisha unaendeshaje sasa bila kufanya kazi yoyote ya kukuingizia kipato?

Barnaba: Mimi kama unavyojua ni prodyuza hivyo nafanya kazi kama kawaida na ninaendelea na vitu vingine na maisha yanaendelea.

Mwandishi: Mashabiki wako wengi wanasema umeyumba toka alipofariki marahemu Ruge hilo unalizungumziaje

Barnaba: Kweli kifo cha Ruge kilinitetemesha sana na kunirudisha nyuma kwa sababu alikuwa ni mtu muhimu sana kwangu lakini Mungu ni mwema maneno yake ya busara yanifanya nisonge mbele siku zote.

Mwandishi: Vipi kuhusu familia maana kuna kipindi tulisikia unataka kuoa baada ya kuachana na mama mtoto wako, Zubeda vipi tayari ushafunga ndoa na mchumba wako Raya?

Barnaba: Mimi na Raya ni kama mtu na mkewe tu maana tumekaa muda mrefu sana lakini Mungu akijalia tutafunga ndoa yetu kubwa na kila mtu atahudhuria.

Mwandishi: Vipi kuhusiana na High Table Studio bado iko chini ya umiliki wako?

Barnaba: Ndio ile ni mali yangu na ndio nafanyia kazi kila kukicha maana ndio maisha yangu ya kila siku.

Mwandishi: Umekuwa mtu wa tofauti sana katika mambo ya kiki kama wanavyofanya wasanii wengine, kwa nini umeamua kuwa hivyo?

Barnaba: Kiki ni kitu kibaya sana, kiki zinaharibu muziki, zinaharibu heshima yako sasa kama mimi ninajua muziki siwezi kufanya kiki kwa sababu najua muziki unataka nini na wala sitaki kujitia doa.

Mwandishi: Lakini ndio inaaminika inamuinua msanii vizuri?

Barnaba: Sio kweli kwa mwanzo watadhani hivyo lakini inamuangusha kabisa.

Mwandishi: Kwa hivi sasa una watoto wangapi?

Barnaba: Wawili ambao ni Stive na Maria.

Mwandishi: Wote umezaa na mama mmoja?

Barnaba: Hapana Ni mama wawili tofauti.

Mwandishi: Mpaka sasa ulipo, muziki wako umekupa faida gani?

Barnaba: Kwa kweli nikisema sijafaidia ni uongo kabisa, nimefaidia mambo mengi na kubwa zaidi watu kunijua kama Barnaba na kutambua nini nafanya na kutambulika mpaka na viongozi wa nchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here