Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe aiombea ushindi Simba SC

0
Nyota wazawa, beki Mohammed Hussein 'Tshabalala' na kiungo Hassan Dilunga wakifanya mazoezi jana kuelekea mchezo na wenyeji, FC Platinums Jumatano ijayo, Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe.

NA SHEHE SEMTAWA

UONGOZI wa Ubalozi wa Tanzania nchini Zimbabwe umeweka wazi kuwa wawakilishi wa Ligi ya Mabigwa barani Afrika, Simba SC wako kwenye mikono salama na kuwahakikishi wa Watanzania kuwa watashinda mchezo wao dhidi ya wenyeji FC Platnum.

Aidha, Benchi la ufundi la Simba, jana, wamekagua Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe ambao utatumika Desemba 23 mwaka huu, katika mchezo wa Ligi hiyo ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji FC Platinum.

Akizungumza na wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa Simba mara baada ya kuwasili siku nne zilizopita nchini humo, Balozi wa Tanzania Prof. Emmanuel Mbena, alisema timu ya Tanzania inapokuwa nje ya Tanzania inawakilisha nchi kwa hiyo wao ni mabalozi wenzake.

Alisema, anaamini kujituma kwao na kuwa na benchi la ufundi zuri, hali hiyo inamfanya ajiamini, asiwe na wasiwasi, kusu suala la ushindi wa timu hiyo ya Simba.

 “Mkurugenzi hatuna wasiwasi, mwalimu hatuna wasiwasi najua tu mtashinda na sisi tuko pamoja nanyi na mwisho nawatakia mafanikio katika mchezo huo,”alisema Prof. Mbena.

Jana benchi la ufundi la Klabu hiyo ya Simba, waligua Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe ambao utatumika Desemba 23 kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji wao FC Platinum.

Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji na msaidizi wake Seleman Matola ambaye ni mzawa kimeshapiga kambi nchini Zimbabwe.

Desemba 18 kiliwasili nchini humo ikiwa ni hesabu za Sven katika kutaka kikosi kiweze kuzoea mazingira ya ugenini.

Kocha huyo, aliweka wazi kwamba wana kazi kubwa ya kufanya ugenini ili kusaka ushindi kwa kuwa lengo ni moja kushinda ili kutinga hatua ya makundi.

“Malengo yetu ni kuona kwamba tunashinda na kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wa kwanza kisha ule wa marudio nao tutapambana kusaka ushindi.

“Wapinzani wetu ni timu kubwa na imara ila haitupi mashaka kwa kuwa nasi pia tupo imara,”alisema Vandenbroeck.

FC PLATINUM

Wakat Simba ikiwa imeweka makazi nchini Zimbabwe siku nne zilizopita kwa ajili ya mchezo huo, uongozi wa timu ya FC Platinum  uliweka wazi kuwa utafanya juu chini kwa kuhakikisha wanapata ushindi wa kutosha ili uwe faida kwao katika mchezo wa marudiano utakaopigwa hapa nchini.

Mchezo wa marudio, unatarajiwa kupigwa Uwanja Mkapa jijini Dar es Salaam ambapo FC Platinum inatarajiwa kuwa Januari 6 mwakani.

FC Platinum ambayo anayochezea Mtanzania, Elias Maguri inatarajia kucheza na Simba katika mchezo wa hatua ya kwanza ya michuano hiyo Desemba 23 katika mchezo ambao Simba itaanzia ugenini.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa timu FC  Platinum, Chido Chizondo, wamejiandaa vizuri kwa kuhakikisha wanapata matokeo makubwa katika mchezo huo kwa kuwa wanatambua ubora wa Simba inapocheza kwenye uwanja wake wa nyumbani.

“Tumejiandaa kupata matokeo mazuri, namaanisha ushindi mkubwa ambao kwetu hauwezi kuwa kikwazo katika mchezo wa marudiano, tunajua kwamba Simba ni bora lakini tutakuwa bora kwa sababu tunaanzia kwetu.

“Nadhani kikubwa ni kwamba tunaelewa Simba ni timu ya aina gani kutokana na kuweza kutumia vyanzo vyetu kufahamu baadhi ya mambo muhimu lakini tunaelewa kuna baadhi ya maofisa wao wameshaingia Zimbabwe ila hatuwezi kuhofia chochote,”alisema Chizondo.

Nyota wa 24 wa Simba wapo nchini Zimbabwe kwa sasa ikiwa ni pamoja na kiungo mkabaji chaguo namba moja kwa Kocha Mkuu, Vandenbroeck, Jonas Mkude.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here