Aweso awataka RUWASA kukamilisha miradi ifikapo Machi 2021

0

NA SHEHE SEMTAWA

WAZIRI wa Maji, Juma Aweso, ameihimiza Bodi ya  Wakala wa Usambazaji wa Maji Vijijini (RUWASA), pamoja na Menejimenti yake kuaininisha miradi yote ya maji vijijini  yenye changamoto na kujua gharama zake na namna ya kuzitatua changamoto hizo.

Aweso aliyasema hayo, wakati alipozungumza na Wajumbe wa Bodi ya RUWASA pamoja Menejimenti katika kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma Jana.

“Hakikisheni mnafanyakazi kwa kushirikiana kama timu moja ya Wizara ya Maji ili tuweze kutekeleza lengo letu la kuwahudumia Watanzania na kuwapatia majisafi, salama na yenye kutosheleza,”alisema Aweso.

“Sisi wiki yetu ya maji, tunakwenda kwenye wiki ya  maji sio wiki ya mapambio wakati father X-Mas anatoa zawadi kwenye X-Mas,  sisi katika wiki ya maji tunataka tutowe zawadi ya maji kwa Watanzania na Rais wetu.

Aweso, aliwataka RUWASA kuhakikisha kuwa ifikapo Machi 2021 miradi yote yenye changamoto iwe imekamefanyiwa kazi na kukamilika kwa kutoa huduma kwa wananchi, yenye uhakika.

Aidha, waziri aliwataka RUWASA kuongeza ushirikianoo katika utekelezaji wa majukumu yao, lengo likiwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo kwa uhakika.

“Nautaka Uongozi wa RUWASA kuaninisha miradi yote iliyokamilika kwa kutumia wataalam wa ndani (Force Account), na kuhakikisha miradi yote ya maji nchini inakuwa endelevu kwa kuunda vyombo vya watumia maji vye uwezo wa kusimamia na kuendesha miradi hiyo,”alisema Aweso.

Aidha, Aweso alisema kuwa kuna haja kwa RUWASA kuimarisha ushirikiano na Chuo cha Maji kwa kuwatumia wataalamu wanaotoka katika chuo hicho katika  usimamizi wa miradi yay a maji wanayotekeleza.

“Mkurugenzi mtu anayekwamisha mchukulie hatua, leteni mawazo tujadiliane pamoja mwisho wa siku tuweze kuisaidia Ruwasa.  Nina Imani mnaweza, Mimi nafasi yangu iko wazi, muda wowote saa yeyote, mwanyekiti mkurugenzi na timu yako njooni tujadiliane, mimi sitaki majungu lakini mawazo ambayo tunakiwa tuyatowe, tuko tayari kufanyakazi na kuweza kusaidia,”alisema Aweso

Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA, Mhandisi Clement Kivegalo alisema moja ya changamoto inayowakabili ni rasimali watu ambapo bado wakala huo unahitaji wataalam.

Alisema katika mwaka wa fedha 2020/2021 RUWASA ilipanga kuelekeza miradi 1,629 na mpaka robo ya kwanza ya mwaka idadi ya miradi iliyokamilishwa ni 222.

Mwenyekiti wa Bodi ya RUWASA Prof. Idrissa Mshiro aliishukuru Serikali kwa kuiwezesha RUWASA kwa namna mbalimbali katika kutekeleza majukumu yake na kumhakikishia Waziri Aweso kuwa RUWASA itahakikisha inatekeleza majukumu yake ipasavyo.

Pia, alisema Bodi iliielekeza RUWASA kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi kwa kutumia wataalam wa ndani (Force Account), ili miradi ikamilike kwa wakati na wananchi waweze kupata huduma hiyo mapema zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here