Askofu Banzi afariki

0

Na Mwandishi Wetu 

Aliyekuwa Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Tanga, Antony Banzi amefariki dunia leo asubuhi Jumapili Desemba 20, 2020.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima amesema amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Katika taarifa hiyo Kitima ametoa pole kwa familia ya jimbo la Tanga na kueleza kuwa taarifa zaidi kuhusu taratibu za mazishi zitatolewa baadaye.

“Baraza linatoa pole kwa familia yote ya jimbo la Tanga na kanisa katoliki Tanzania kwa msiba huu mzito. Tunamuombea kwa Mungu ili roho yake ipumzike kwa amani mbinguni pamoja na watakatifu,” amesema.

Askofu Banzi alizaliwa Oktoba, 1946. Mwaka 1994 aliwekwa wakfu na Kardinali Polycarp Pengo kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Tanga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here