Askari walimvyomnusuru Bocco na kipigo

0

NA MWANDISHI WETU

KATIKA hali ya kushangaza mshambuliaji wa Simba, John Bocco, juzi alinusurika kupigwa na mawe na mashabiki wa timu hiyo kufuatia kitendo cha kukosa penalti katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting ambao walichapwa bao 1-0.

Bocco alikosa penalti dakika ya 78 kwa shuti lake kugonga mwamba hali ambayo iliwakasirisha mashabiki kwa kuwa mchezo uliopita walifungwa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons. 

Tukio hilo ambalo, lilishuhudiwa na baadhi ya vyombo vya habari mara baada ya mchezo huo, kwa mashabiki wakiwa wamejazana upande wa kutokea uwanjani huku wakidai wanamtaka Bocco na wengine wakiwa wameshika mawe mkononi.

Kitendo cha mashabiki hao kilipelekea Polisi kulazimisha basi la timu hiyo kuingia ndani ya uwanja kwa lengo la kuwatoa wachezaji huku ulinzi ukiwa umeimarishwa lakini haikuweza kuwafanya mashabiki hao kutoka katika eneo.

 Hata hivyo basi la timu hiyo liliwachenga na kupitia kwenye geti lingine linalotazama na Uwanja wa Mkapa na kuondoka uwanjani hapo.

Juzi, Bocco aliwaomba radhi viongozi na wanachama wa mabingwa hao wa ligi kuu Tanzania bara kwa matokeo mabaya waliyoyapata katika mechi mbili mfululizo zilizopita.

Bocco ameandika kupitia mitandao yake ya kijamii alisema wanafahamu namna viongozi na wanachama wanavyoiunga mkono katika kila nyanja na wanaumizwa kwa matokeo hayo.

Nahodha huyo ambaye juzi alikosa mkwaju wa penati dhidi ya Ruvu Shooting ambao walipoteza kwa kipigo cha bao 1-0, amewaahidi viongozi na wanachama kwamba watajituma maradufu ili waanze kushinda michezo ijayo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here