Askari kizimbani kwa kuiba kasha la fedha

0

Na Devotha Fulugunge

ASKARI mmoja  William Komba (36) amefikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kujibu shtaka linalomkabili la wizi wa sanduku la amana na usalama lenye thamani ya Sh  Milioni 1.5 kwa kutumia silaha katika shule ya Msingi na sekondari ya Capstone.

Komba ambaye ni askari polisi anayeishi katika nyumba za polisi  Kunduchi , amefikishwa mahakamani hapo jana  mbele ya Hakimu Mkazi  Lilian Silayo.

Awali, akisoma shtaka ilo mbele ya Mh.Silayo Wakili wa Serikali Hilda Katto alidai Juni 11, 2020 mshtakiwa aliiba sanduku la huduma ya Kwanza Lenye thamani ya Sh.milioni 1,500,000 eneo la Goba Chaurembo, Ubungo jijini Dar-es-Salaam Mali ya Capstone kwa kutumia silaha.

Aliongeza kuwa mda mfupi baadae, aliwatishia askari wawili, F.1071 D/CPL Hamza na H.9709 D/C Fredrick kwa bastola waliyokuwa wanapambana ili kurudisha sanduku la shule hiyo.

Naye mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo mbele ya Mahakama, wakili alisema upelelezi bado aujakamilika na kuomba tarehe nyingine kwa kusikiliza hoja za awali.

Kwa upande wa Hakimu baada ya kusikiliza shtaka hilo alisema kosa alina dhamana  kwa mujibu wa sheria.Kesi ilihahirishwa na mshtakiwa alirudishwa rumande Hadi Novemba 19 mwaka huu kwa kutajwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here