Asilimia 80 Pochetino kutangazwa Kocha Mkuu Man U

0

LONDON, Uingereza

INAELEZWA kuwa kocha anayefuata ndani ya Klabu ya Manchester United ni Mauricio Pochentino ambaye kwa sasa hana timu baada ya kufutwa kazi ndani ya Klabu ya Spurs.

Ole Gunnar Solkjaer ambaye ni Kocha Mkuu wa Manchester United kwa sasa yupo kwenye presha kubwa ya kufutwa kazi kutokana na mwendo wake wa kusuasua ndani ya timu hiyo ambayo inahitaji mafanikio makubwa.

Ushindi wake wa mabao 3-1 dhidi ya Everton kwa kiasi fulani umempa ahueni kocha huyo lakini bado fukuto linaendelea kwa kuwa kazi bado ipo hasa kwenye upande wa muunganiko na namna kikosi chake kinavyopambana kusaka matokeo.

Kuhusu hali hiyo Ole alisema “Mimi nipo kwenye kazi yangu ambayo nimepewa na mkataba wangu na mabosi zangu ni wa kudumu hivyo ninafanya kazi kwa uwezo wangu ikiwa itatokea tofauti basi itajulikana.

“Muda mwingine tunashindwa kupata matokeo haina maana kwamba wachezaji hawajitumi hapana ni matokeo kama ilivyo matokeo mengine licha ya kwamba hakuna anayependa kupoteza,”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here