Argentina kujadili picha ya Maradona kutumika kwenye fedha yao

0

BUENOS AIRES, ARGENTINA

SENETA Norma Durango wa Argentina amewasilisha muswada katika Bunge la nchi hiyo akipendekeza picha ya lejendari wa soka duniani, Diego Maradona, aliyefariki Novemba 25, 2020, iwekwe kwenye fedha za noti za nchi hiyo (Peso 1,000 sawa na Sh 27,600.)

Durango, alisema lengo ni kumuenzi nyota huyo kwa heshima aliyolipa taifa hilo mwaka 1986 baada ya kuiwezesha Argentina kutwaa Kombe la Dunia na kuiandika historia ya nchi hiyo katika ramani ya soka duniani.

Noti hiyo itaonyesha sura ya Maradona huku upande mwingine ikionyesha goli maarufu alilofunga kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Uingereza 1986.

Maradona ambaye aliwahi kuchezea vilabu vikubwa duniani ikiwemo Napoli ya Itali na FC Barcelona vilabu vingine kabla ya kustaafu soka kufuatia kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya, alifariki kwa tatizo la shambulio la moyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here