Amber Lulu atoa ya moyoni jinsi anavyompenda Diamond

0

NA MWANDISHI WETU

SUPASTAA mkubwa wa muziki barani Afrika, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amemponza sexy lady anayekiwasha kwenye Bongo Fleva, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’.

Amber Lulu alikiambia chombo kimoja cha habari kuwa, amejikuta akishambuliwa kila kona, lakini anawashangaa watu wanaomshambulia kwa kuwa tu ameeleza hisia zake kwamba anamzimikia Diamond au Mondi kutoka moyoni mwake.

Amber Lulu anasema kuwa, yeye haoni kitu cha ajabu kueleza hisia zake kwamba anampenda Mondi kwani ni jambo ambalo limempata bila kutegemea wala kupanga.

Mwanadada huyo mwenye umbo lake mjini anasema kuwa, watu wengi wanabana hisia zao ndani ya mioyo yao na mwisho wake wanapata presha zisizo za msingi. 

Anasema kuwa, kwa upande wake yeye hawezi kujibana kama anampenda mtu anasema ukweli kwa sababu siyo kitu cha ajabu duniani.

  “Nimeeleza hisia zangu juu ya mtu ninayempenda na anayeninyima usingizi, mtu kusema unampenda mtu fulani siyo kitu kigeni kwa sababu hakuna cha ajabu na ndiyo maana unakuta mtu anadondoka na kufa, kisa kabanabana hisia zake muda mrefu.

“Mimi siwezi kujibana, naweka wazi ninampenda Diamond kwelikweli, sitanii na ananikosesha usingizi sana,” anasema Amber ambaye kwa sasa anadai ana upweke kwa kuwa hana mpenzi.

Miezi kadhaa iliyopita, kwa mara ya kwanza Amber Lulu alieleza ni kwa namna gani amejikuta kwenye wakati mgumu kwa kumpenda Mondi na yupo tayari kumzalia idadi yoyote ya watoto anaowataka.

Lakini alidai kuwa kuna watu wamekuwa wakimuwekea kauzibe asikutane na jamaa huyo uso kwa uso ili amueleze juu ya mapenzi tele aliyonayo kwake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here