Aliyekuwa Mwenyekiti UVCCM ateuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya

0

Na Mwandishi Wetu 

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Sadifa Juma Khamis amerudi kwenye anga za uongozi baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kusini-Unguja na Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi .

Sadifa ni kada mwandamizi wa CCM akiwa amewahi kushika wadhifa wa Mwenyekiti wa UV-CCM na pia Mbunge wa Donge kuanzia 2015 hadi 2020.

Dk Mwinyi jana alitangaza jana kufanya uteuzi wa wakuu wa wilaya 10 visiwani Zanzibar ikiwa ni mwendelezo wake wa kuteua viongozi wa serikali yake tangu alipochaguliwa Oktoba, mwaka huu.

Taarifa ya Ikulu ya Zanzibar ilieleza wengine walioteuliwa ni Aboud Hassan Mwinyi kuwa Mkuu wa Wilaya Kaskazini A na Kassim Haidar Jabir kuwa Mkuu wa wilaya Kaskazini B.

Pia Dk Mwinyi amemteua aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B Rajab Ali Rajab kuwa mkuu wa wilaya ya Mjini na aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Wete Mohhamed Mussa Seif ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Micheweni

Vilevile amemteua Khamis Mbeto Khamis kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A, Mgeni Khatib Yahaya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete na Abdullah Rashidi ali kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake.

Kadhalika aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kati, Hamida Mussa Khamis ameteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Magharibi B huku aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Marina Joel Thomas ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kati.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here