Aliyeandaa tiketi za ufuska Dar kizimbani

0
Mshtakiwa Faraji Omary (26) akiwa ameficha uso wake ili asipigwe picha, katika Mahakama ya Hakimu Kisutu, baada ya kusomewa mashtaka manne likiwemo la kusambaza picha za ngono.

Na DEVOTHA FULUGUNGE

Faraji Omary amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa makosa manne yanayomkabili  likiwemo la kuchapisha picha chafu  za ngono.

Omary (26), mkazi wa Mbagala alifikishwa Mahakama hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Rashid Chaungu.

Awali Wakili wa Serikali Adolf Ulaya kupitia hati ya mashtaka alidai kuwa,mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka manne ambayo ni kuchapisha ponografia, kusambaza maudhui machafu, kusambaza picha chafu na kukutwa na machapisho yenye maneno machafu.

Wakili ulaya aliendelea kudai kuwa katika shtaka la kwanza kati ya  Desemba 4 na 14, mwaka huu jijini Dar-es-Salaam mshtakiwa alituma video na picha za ponografia kupitia WhatsApp kwa namba ya simu ya  0747644457.

Katika shtaka la pili, Wakili alidai kati Disemba 10 na 12, mwaka huu eneo la Kariakoo jijini Dar-es-Salaam mshtakiwa alitengeneza tiketi zenye maneno machafu yanayoharibu maadili ya umma.

Shtaka la tatu Wakili aliendelea kudai Disemba 12, mwaka huu eneo la Kariakoo jijini Dar-es-Salaam mshtakiwa alitengeneza tiketi zenye maneno machafu kwa ajili ya kufanya biashara na mtu aliyejulikana kwa jina la Aisha Feruz au “Sex Aisha”.

Shtaka la nne ni kuwa, Disemba 24, mwaka huu wilaya ya Ilala  Kariakoo jijini Dar-es-Salaam mshtakiwa alikutwa na tiketi zenye maneno machafu aliyokusudia kusambaza kwa kuziuza.

Mshtakiwa alikana kutenda makosa hayo na kwa upande wa Jamhuri ulidai upelelezi bado haujakamilika na kuomba tarehe nyingine na kwamba hauna pingamizi kwa upande wa dhamana.

Hakimu Chaungu alitaja masharti ya dhamana ambapo mshtakiwa alitakiwa kuwa na wadhamini Wawili ambao walitakiwa kusaini hati ya Sh. Milioni tano kila mmoja sambamba na barua za utambulisho.

Mshtakiwa alirudishwa rumande kwa kuwa hakukidhi masharti ya dhamana na Hakimu Chaungu aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 11, 2021.

Mbali na kupata mwanamke wa kuburudika naye, mwanaume ambaye angehudhuria sherehe hiyo angepewa chumba, kuogelea na kupata huduma nyingine.

Itakumbukwa hivi karibuni katika mitandao ya kijamii kulikuwa na kipande cha video kikitangaza tiketi kwaajili ya sherehe za ufuska iliyokuwa imepangwa kufanyika Mbezi Beach Desemba 23, 2020 kabla ya Polisi kuingilia kati na kuzima shughuli hiyo.

Katika video hiyo ilisikika sauti ya mwanamke akinadi tiketi na huduma atakayopata mtu atakayenunua.

Mbali na kupata mwanamke wa kuburudika naye, mwanaume ambaye angehudhuria sherehe hiyo angepewa chumba, kuogelea na kupata huduma nyingine.

“Hizi ndio tiketi zetu… hii ni ya Sh300,000 unapata wanawake wawili wa kufanya nao mapenzi na ya Sh100,000 unapata mwanamke mmoja wa kufanya naye mapenzi. Kwenye hii tiketi utapata chumba, utaogelea na shoo yangu ya (anaitaja), wote mnakaribishwa Mbezi Beach private house,” alieleza mwanamke huyo kwenye video hiyo.

Hata hivyo mahakamani hapo haikubainishwa moja kwa moja kwamba mshtakiwa huyo ndiye anahusika na video hiyo au kama ni nyingine.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here