Ajali yamfanya Belle 9 kuimba Injili

0

NA MWANDISHI WETU

MKALI wa muziki wa RnB Belle 9 amesema ameamua kuimba wimbo wenye mahadhi ya Injili baada ya kujitafakari ndani ya nafsi yake kufuatia tukio la kupata ajali ya gari siku ya Septemba 7, akiwa na wasanii wengine ambao ni Bonge la Nyau na Lulu Diva.

Belle 9 alisema eneo hilo ambalo amepata ajali ni ngumu sana watu kusalimika ila yeye amefanikiwa kutoka salama ndiyo maana akaimba wimbo huo wa injili ili kumshukuru Mungu.

“Baada ya kupata ajali nilitumia muda mwingi kujitafakari ndani ya nafsi yangu, niliambiwa  eneo nililopata ajali watu wengi huwa wanapotea kabisa, kwahiyo matokeo ya kuimba ule wimbo ni baada ya kutoka salama na kutoa shukrani, nimeujua ukubwa wa mungu na sasa hivi maisha yangu yamebadilika”

Belle 9, Bonge la Nyau na Lulu Diva walipata ajali ya gari maeneo ya Chalinze wakati wanatoka kwenye kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ilolo, Mkoani Iringa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here