Nyota wa Liverpool na Timu ya Misri, Mohamed Salah ‘Mo Salah’ anatarajia kuvaa kiatu maalum kilichotengenezwa kwaajili yake kutoka katika kampuni ya Adidas kwenye mchezo wa Klabu Bingwa Ulaya baada ya kufanikiwa kufunga jumla ya magoli 100 siku ya Jumamosi mbele ya Everton.
Salah anakuwa mchezaji wa kwanza kufikisha idadi hiyo ya magoli Liverpool tangu mara ya mwisho kufanywa hivyo na Steven Gerrard mwaka 2008.
Mmisri huyo anakuwa nafasi ya tatu kwenye orodha ya wachezaji 17 wa Liverpool waliyofikia idadi hiyo ya magoli kutokana na idadi ya michezo aliyocheza, wakwanza akiwa Roger Hunt (akicheza michezo 144) wapili Jack Parkinson (153) na watatu ni Salah akifikisha idadi hiyo ya magoli kwenye michezo yake 159 aliyocheza.
Katika kusherehekea idadi hiyo ya magoli Adidas imemtengenezea kiatu maalum mchezaji huyo kutoka Afrika ambacho atakivaa siku ya Jumatano kwenye mechi yao ya Klabu Bingwa dhidi ya Ajax.