Abdi Banda kutimkia Uturuki

0

NA MWANDISHI WETU

NYOTA wa Klabu ya Highlands Park ya Afrika Kusini ABDI Banda, ameweka wazi kuwa anasubiri ofa ya timu  moja ya nchini Uturuki baada ya kurejea Tanzania kutokana na timu hiyo aliyokuwa akiitumikia awali kupata bosi mpya jambo lilifanya mfumo kubadilika.

Beki huyo mzawa ambaye alicheza pia Baroka FC aliweka wazi kuwa kuna mawasiliano ya pande mbili hivyo mambo yakienda sawa anaweza kusepa.

Msimu wa 2014-17 alicheza ndani ya Klabu ya Simba ambapo aliibuka huko akitokea Klabu ya Coastal Union. 

Ndani ya Baroka FC alicheza jumla ya mechi 41 na alitupia mabao manne.

Kwenye timu yake ya Highlands Park alicheza jumla ya mechi 4.

“Kuna mawasiliano ya pande mbili kwa sasa kati ya meneja wangu na mabosi wa nchini Uturuki hivyo mambo yakiwa sawa nitajua wapi nitakapokwenda kucheza,”alisema Banda.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here