Mtoto wa Garner kutoa wimbo na Lady Jay Dee

0

Na Mwandishi Wetu

MKONGWE wa Bongofleva Judith Wambura maarufu Lady Jay Dee amesema tayari wameanza maandalizi ya kuachia kazi mpya ambayo atashirikiana na mtoto wa mtangazaji Gadner aitwaye Karen.

Jide amethibitisha hilo baada ya kuonekana kuzagaa kwa picha zikimuonyesha akiwa na Karen huku akidai picha hizo walipiga wakati wakiwa studio.

“Ni kweli kuna kazi mpya inakuja mimi na mwanangu Karen, ni moja ya mipango ambayo tulijiwekea muda mrefu na nadhani huu ni wakati sahihi wa kukamilisha hili”alisema Jide.

Aidha, Jide aliongeza kuwa kufanya kazi na Karen hakumaanishi kushinikizwa na ukaribu wake na baba yake bali ni sehemu ya majukumu yake kama msanii kuendeleza shughuli zake za kimuziki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here