Ureno kuisaidia Msumbiji kupambana na wanamgambo

0

Ureno imejitolea kuisaidia Msumbiji kupanga mkakati na kuiwezesha jeshi la nchi hiyo kukabiliana na wanamgambo wa Kiislamu wanaotishia usalama katika Mkoa wa kaskazini wa Cabo Delgado wenye utajiri wa gesi.

Mwezi uliyopita wanamgambo waligeuza uwanja wa michezo kuwa “kichinjio”, ambako walikata watu vichwa na miili, kwa mujibu wa ripoti.

Waziri wa Ulinzi wa Ureno, Joao Gomes Cravinho, amesema kundi la wanajeshi wa nchi hiyo kuanzia mwezi ujao litaanza kufanya kazi na wenzao wa Msumbiji.

Wikiendi iliyopita Bw. Gomes Cravinho alikamilisha ziara ya kikazi ya siku tatu katika nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika.

Alisema Ureno, ambayo itatoa Rais wa Muungano wa Ulaya kuanzia mwaka 2021, itaunga mkono ombi la Msumbiji la kupewa msaada ambalo tayari limewasilishwa Brussels.

Ghasia katika mkoa wa Cabo Delgado umesababisha mzozo wa kibinadamu, huku zaidi ya watu 2,000 kuuawa na wengine 560,000 kufurushwa makwao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here