Msanii wamuziki wa kizazi kipya Zuhra Othman (ZUCHU) kesho Disemba 31 atafanya onyesho la KUFUNGA mwaka katika fukwe za SAROVA WHITESANDS nchini Kenya onyesho lililopewa jina la magic night.
ZUCHU atatumbuiza mubashara na bendi ya H_ART THE BAND itafata katika onyesho hilo huku washereheshaji wakiwa ni mc Jessy, mwalimu Rachel na Dj Ramoz, ambapo onyesho hilo litaanza saa Moja usiku mbele ya fukwe hizo.
Kupitia ukurasa wake aliwaalika na kuwataarifu wakazi wa mombasa kuhusu usiku ambao atakuwa akitoa burudani hiyo. “hellow mombasa habarigani mombasa asalamu aleikum mombasa it’s me your girl Zuchu na Niko hapa kuwapa taarifa tarehe Thelasini na mojamwezi huu on new years event myself I will be performing kwenye Hotel SAROVA WHITESANDS beach resort me and my band we’ll be there to give you a good new years event”