14 wafariki, 13 wajeruhiwa katika ajali ya gari Singida

0

Watu 14 wamepoteza maisha na wengine 13 wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea maeneo ya Kiini cha Mkiwa mkoani Singida baada ya gari ndogo ya habiria kugongana uso kwa uso na Lori lililokua linatoka Dar es Salaam kwenda Kahama.

RPC Singida, Sweetbert Njewika,  amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo  kwa kile  alichodai ni uzembe wa dereva wa gari  ya abiria ambae nae amefariki alikua mwendo kasi na kulipita Lori kwa kulichomekea  bila kuwa makini.

Majeruhi wanapatiwa matibabu hospitali ya Manyoni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here